RAIS wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville), Mhe.  COLLINET MAKOSSO Anatole. Mhe. Anatole alipokea ujumbe huo wa maandishi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Congo , Mhe. Denis Sassou Nguesso ambaye alikuwa kijijini kwao kushiriki mazishi ya kaka yake.

Tukio hilo lilifanyika jijini Brazzaville Aprili 14, 2025 na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili.

Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...