Na John Luhende

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuhakikisha 
mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibada-Mwasonga Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam unakamilika kwa wakati kwa mujibu wa mkataba na kwa ubora unaotakiwa.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara hiyo ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania.

Aidha amesema niwajibu wa wanananchi kutoa ushirikiano kwa Wizara na Mkandalasi ikiwemo ulinzi wa vifaa vya ujenzi kwani kukosekana na ulinzi Madhubuti kunaweza kuchangia kuzolotesha kasi ya kukamilika kwa mradi huo.

Kadhalika Dkt Mwinyi amewataka Watanzania Kuendelea kulinda Amani ili Taifa lipige hatua zaidi za Maendeleo na kwa kuwa huu ni Mwaka wa Uchaguzi amewataka kutumia haki yao kuchagua Viongozi na kuhakikisha Uchaguzi hauwi chanzo cha kuhatarisha Amani ya Nchi na kuweka Mbele Maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa aliyemwakilisha Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mingi ya barabara nchi nzima, huku barabara ya Kibada–Mwasonga–Kimbiji ikitajwa kuwa ya kimkakati kwa ajili ya kukuza uchumi wa Wilaya ya Kigamboni.

Awali Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, amesema mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya Estim Construction kwa gharama ya Shilingi bilioni 83.8 na unatarajiwa kukamilika Disemba 2025, akieleza kuwa utekelezaji wake ukiwa umefikia asilimia 30 hadi sasa.

Mradi huo tayari umezalisha ajira 331, kati ya hizo 326 ni Watanzania na watano 5 ni raia wa kigeni. Serikali inaendelea kushughulikia ombi la mkandarasi kuhusu nyongeza ya muda wa miezi mitano kufuatia changamoto za kimkataba.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuleta neema ya maendeleo mkoani humo na kusisitiza kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu cha uchumi wa Kigamboni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo April 25 akifungua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi Wa Barabara ya Kibada-Mwasonga Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania.aziri wa Mawasiliano na Teknolojia Jerry Silaa ,akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega,


Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, akitoa taarifa ya ujenzi wa Barabara ya Kibada-Mwasonga Wilaya ya Kigamboni, mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyikatika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi
Mstahiki Meya wa Manispaa yaKigamboni Ernest Mafimbo wapili kutoka kulia akifuatilia wengine ni viongozi wa viongozi mbalimbali wakifutilia tukio la uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Kibada-Mwasonga Wilaya ya Kigamboni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,Albert Chalamila akizunguza kabla ya hotuba ya Mgeni Rami Dkt Hussein Alli Mwinyi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...