-Ukarabati uwanja wa Benjamini Mkapa wafikia asilimia 80

Na Mwandishi wetu - Dar es Salaam

Uwanja wa Benjamin Mkapa umeendelea kukarabatiwa kwa kasi, ambapo hadi sasa kazi hiyo kubwa imefikia asilimia 80 ya utekelezaji. Ukarabati huu ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambayo imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya michezo nchini.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Boniface Tamba, kazi kubwa tayari imefanyika ikiwemo kubadilisha viti vyote 62,000 na kuweka vipya vya kisasa vinavyolingana na rangi za bendera ya Taifa — kijani, njano, nyeusi na bluu — kama ishara ya uzalendo na uimara wa taifa.

Aidha, maboresho ya mfumo wa umeme na taa yamekamilika kwa kiwango kikubwa, ambapo taa mpya za kisasa zilizowekwa zinakidhi viwango vya kimataifa, hatua inayolenga kuufanya uwanja huo kuwa tayari kwa mashindano ya kimataifa pamoja na matukio makubwa ya kitaifa.

Eneo la michezo la Benjamin Mkapa linahusisha sehemu kuu tatu ambazo ni:

• Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 62,000,

• Uwanja wa Uhuru unaochukua watu 22,000,

• Na kituo maalum cha michezo kwa ajili ya mapumziko na burudani kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...