Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imezindua rasmi kanuni za uongezaji virutubishi katika vyakula hatua inayolenga kuboresha afya na lishe ya Watanzania. 


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo aliyekua mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Silaoneka  Kigahe (Mb) amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata chakula chenye virutubishi muhimu kwa ustawi wa afya yake.




Kanuni hizi mpya zinatokana na mkataba wa makubaliano uliofanyika Septemba 2022 kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na wakuu wa mikoa ambapo ilikubaliwa kuweka mikakati thabiti ya kupunguza udumavu na utapiamlo kwa kuongeza virutubishi kwenye vyakula kama unga wa ngano,  unga wa mahindi  na chumvi vimetajwa kuwa ni vyakula vinavyohitaji kurutubishwa zaidi.


Serikali pia imeazimia kuwezesha teknolojia za uongezaji virutubishi kupitia viwanda vya ndani, hatua inayorahisisha upatikanaji wa lishe bora. Ambapo kupitia Kiwanda cha Sanku Tanzania, ambacho kinazalisha tani 150 za virutubishi kwa mwaka kinatosheleza mahitaji ya nchi nzima huku sehemu ya uzalishaji wake ikiuzwa katika nchi jirani kama Ethiopia, Kenya na Uganda.




Kwa upande wake muwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Saitole Lazier ameeleza kuwa suala la urutubishaji wa vyakula sio geni nchini, kwani mpango wa kwanza ulizinduliwa mwaka 1994 chini ya Rais wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi. 

Mpango huo ulilenga kuongeza madini joto kwenye chumvi ili kuzuia madhara yanayotokana na upungufu wa madini hayo, kama vile matatizo ya ukuaji wa ubongo kwa watoto kabla ya kuzaliwa na ugonjwa wa shingo kuvimba (Goiter).


Mkuu wa Wilaya ya Ruvuma, Kapenjama Ndile akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, amesema mkoa  umeweka mikakati mbalimbali ya kuboresha afya na lishe ambapo Moja ya hatua hizo ni pamoja na kampeni za utoaji wa chakula mashuleni kwa zaidi ya asilimia 80 na mpango wa mwaka 2025-2030 wa kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa kuhamasisha ufugaji wa kuku na samaki pamoja na kilimo cha mbogamboga mashuleni.



Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Luis, ameeleza kuwa utafiti wa afya ya uzazi na mtoto wa mwaka 2022 umebaini kuwa kiwango cha udumavu katika mkoa huo ni asilimia 35.6 kiwango ambacho ni juu ya matarajio ya asilimia 24.

 Serikali inalenga kupunguza kiwango hicho hadi kufikia asilimia 17 ifikapo mwaka 2030 kwa kuongeza uhamasishaji wa lishe bora na utekelezaji wa programu shirikishi.



Kutoka taasisi ya Mwanangu Development Tanzania (MWADETA), Walter amesema kuwa tatizo la watoto kuzaliwa na mgongo wazi na vichwa kujaa maji limekuwa changamoto kubwa nchini kutokana na upungufu wa madini joto. Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya lishe imeandaa mikakati madhubuti ya kuhakikisha lishe bora inapatikana ili kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa na changamoto hizo.


Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania wanatumia chumvi iliyorutubishwa kwa madini joto huku virutubishi kama madini chuma, zinki, vitamini B12, na vitamini A vikiongezwa kwenye vyakula vingine.

Serikali kupitia uboreshaji wa lishe inalenga kupunguza vifo vya akina mama na watoto hasa wale wanaokosa kinga za mwili na wanaozaliwa na matatizo ya ukuaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...