Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao nchini imetangaza kushiriki maandalizi ya Mtoko wa Pasaka utakaofanyika Aprili 20,2025 katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini  Dar es Salaam, ikilenga kuwaunganisha Watanzania kupitia nyimbo, maombi, na kutoa misaada kwa kina mama wajawazito

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam , Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Steven Mengele  almaarufu Steve Nyerere, amesema kuwa tukio hilo litakuwa maalum kwa ajili ya kuliombea Taifa na pia kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mwaka huu wa uchaguzi,pia Taasisi itatoa msaada kwa kina mama wajawazito katika hospitali zote za wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea kilele cha Pasaka.

 "Amani tuliyopewa na Mungu lazima tuilinde kwa gharama yoyote, Maombi yana nguvu kuliko mtutu wa bunduki, akina mama sasa hivi ndio wanaobeba taifa, Hii fursa ya kuwasaidia ni sehemu ya kazi yetu kama taasisi yenye lengo la kuongelea na kugusa maisha ya Watanzania kwa vitendo",amefafanua 
Steve 

Mmoja wa Waimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchin Christina Shusho akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mtoko wa Pasaka utakaofanyika Aprili 20,2025 katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini  Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...