Dar es Salaam, Mei , 2025 — Benki ya Absa Tanzania imethibitisha kwa mara nyingine nafasi yake kama mshirika mkuu katika maendeleo ya uongozi wa kifedha katika ukanda wa Afrika Mashariki, baada ya kudhamini kwa mafanikio Mkutano wa 10 wa Maafisa Wakuu wa Fedha (CFO), uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Serena uliwaleta pamoja zaidi ya wataalamu 100 waandamizi wa masuala ya fedha (CFOs) kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, ambapo walibadilishana uzoefu, kujadili mitazamo mipya na kuimarisha mahusiano ya kitaaluma katika sekta ya fedha.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, alisema udhamini wa benki ya ABSA unaendana na dhamira ya kuendeleza Afrika kwa kusaidia taasisi na viongozi wake wa kifedha (CFOs).

“ABSA Bank Tanzania tukiwa kama wadhamini wakuu wa mkutano huu, tunatambua nafasi nyeti ya viongozi wa fedha (CFOs) katika kusuka mustakabali wa taasisi mbalimbali barani Afrika Mashariki; Nafasi ya CFO imepanuka zaidi ya usimamizi wa kifedha wa jadi; sasa inahusisha ubunifu, mageuzi ya kimkakati na uundaji wa thamani ya muda mrefu.” Alisema Bw. Obedi Laiser.

Alibainisha kuwa benki hiyo inaendelea kutoa suluhisho mahususi ya kifedha na ushauri wa kimkakati ili kusaidia taasisi mbalimbali kustawi katika mazingira ya kiuchumi yenye changamoto nyingi.

“Tupo tayari kushirikiana na maafisa wa fedha kwa kuwapatia maarifa, mitaji na utaalamu utakaowasaidia kufanikisha malengo yao na kufungua fursa mpya za ukuaji,” aliongeza Bw. Laiser.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na mabadiliko ya nafasi ya CFO, mageuzi ya kidijitali, ujumuishaji wa masuala ya mazingira, jamii na utawala bora (ESG), pamoja na mbinu bora za ukuaji wa kimkakati na usimamizi wa mitaji.

Kwa mujibu wa waandaaji, mkutano huo ulikuwa jukwaa muhimu kwa wataalamu wa fedha kuandaa mbinu za kukabiliana na changamoto zinazoikumba sekta hiyo, sambamba na kuimarisha mwelekeo wa ukuaji endelevu wa biashara katika ukanda huu wa Afrika.

Ushiriki wa Absa Tanzania unaenda sambamba na kauli mbiu yake ya “Stori yako ina thamani” kuwawezesha waafrika kupitia ushirikiano wa kimkakati, ubunifu na uongozi wa fikra. Ikiwa na mtandao mpana na uliojiimarisha unaovuka nchi zaidi ya 10 barani Afrika pamoja na ofisi zake London, New York, Namibia na Nigeria, Absa inaendelea kuwa muhimili muhimu katika kukuza uchumi na ujumuishaji wa kifedha.

Mkutano huo ulifungwa kwa wito kwa viongozi wa fedha Afrika Mashariki kuendelea kujifunza, kushirikiana na kuwa wabunifu ili kujenga uthabiti katika mazingira ya kifedha yanayobadilika kwa kasi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...