Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika la Mapinduzi ya kijani Afrika (AGRA),pamoja na mfuko wa.mabadiliko ya tabia nchi (GCF),wamezindua rasmi mradi wa RE-GAIN ambao utasaidia kupunguza upotevu wa mazao ya chakula katika maeneo mbalimbali hapa nchini katika msimu wa mavuno.

Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,mikoa ya Kanda ya Kati pamoja na ile ya Magharibi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, jijini Dodoma Mkurugenzi wa masoko na usalama wa chakula kutoka Wizara ya Kilimo,Gungu Mibavu amesema mradi huo kwa hapa nchini umelenga kusaidia katika mazao ya Mahindi na Mpunga ambavyo hutumiwa na jamii ya watu mbalimbali.

Mibavu amesema lengo la kuzindua mradi huo,ni kutaka kupunguza asilimia 30 hadi 40 ya upotevu wa mazao ya Mahindi na Mpunga unaotokea kipindi cha mavuno katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

"Tunawashkuru sana AGRA,Kwa kazi kubwa wanayofanya ili kuhakikisha sekta ya kilimo inazidi kupiga hatua,lakini pia wanasaidia kuangalia usalama wa chakula,mradi huu utakwenda kupunguza upotevu wa mazao ya chakula,"alisema Mibavu.

Amesema kumekuwa na upotevu wa asilimia 30 hadi 40 kwenye mazao ya mahindi na Mpunga kabla na baada ya mavuno na chakula hupotea kuanzia wakati wa kuvuna mpaka kwenye kuhifandhi hivyo mpango huu wa RE-GAIN unaenda kuisaidia nchi katika kukabiliana na upotevu wa mazao katika nyanja zote.

Mbali na hilo amesema mradi huo pia unalenga kwenda kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo huathiri mara kwa wakulima wa mazao mbalimbali hapa nchini.

Naye Mkurugenzi Mkaazi wa AGRA Vianey Rweyendela amesema Mpango wa RE-GAIN unalenga kwenye mazao mawili mpunga na mahindi na utatumia mbinu kadhaa kama kukuza teknolojia za kisasa katika Kuimarisha upatikanaji wa masoko.

Mbali na hilo Rweyendela amesema mradi huo pia una mpango wa kujenga uwezo kwa kuwapatia wakulima mafunzo ya kina kuhusu mbinu bora za uvunaji,utunzaji baada ya mavuno, na uhifadhi wa mazao baada ya mavuno.

"Huu mradi una umuhimu mkubwa sana kwenye sekta ya kilimo utasaidia kupunguza upotevu wa mazao katika maeneo mbalimbali ambapo utatekelezwa,"alisema Rweyendela.

Amesema pia mradi huu unatekelezwa katika nchi saba Barani Afrika,ikiwemo Tanzania, Malawi,lengo ikiwa ni kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza ustahimilivu wa sekta ya kilimo dhidi ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa/tabia nchi na kuboresha maisha ya wakulima wadogo.

Rweyendela amesema,mkutano mkutano huo umekutanisha wadau muhimu kutoka wizara za serikali, sekta binafsi, na mashirika ya maendeleo ili kuweka mifumo madhubuti ya uratibu na ufuatiliaji, ikiwa ni mwanzo wa safari ya miaka mitano ya kuboresha mifumo ya chakula na mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hapa nchini.

Naye Afisa Kilimo kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bernard Libata aliishkuru AGRA na GCF kutokana na kuzindua mradi huo ambapo alisema unakwenda kusaidia wakulima kupunguza upotevu wa mazao ya chakula.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...