Na Jane Edward, Arusha

Wakulima wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wanaojishughulisha na kilimo cha maharage na mahindi wameshauriwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti, zenye wingi wa virutubisho ikiwemo madini ya chuma na zinki pamoja na vitamini A, kwa ajili ya kupambana na magonjwa mbalimbali yakiwemo utapiamlo, uoni hafifu pamoja na tatizo la udumavu ambalo limekuwa likiathiri asilimia kubwa ya watoto barani Afrika ikiwemo Tanzania.

Ushauri huo umetolewa na Mtaalamu wa Magonjwa na Afya ya Mimea kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Seliani, Dkt. Edith Kadege, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mashamba ya utafiti wa kituoni hapo.

Dkt. Edith Kadege amesema matumizi ya mbegu hizo yanasaidia kuongeza tija ya kilimo kwa wakulima huku yakichangia kuboresha afya ya jamii kwa kupunguza magonjwa yanayotokana na ukosefu wa virutubisho kwenye mlo wa kila siku.

Aidha, baadhi ya watafiti wa kilimo kutoka kituo hicho wameeleza mafanikio yaliyofikiwa kutokana na uhawilishaji wa teknolojia bora za kilimo kwa wakulima. Teknolojia hizo ni pamoja na mbegu bora zinazokinzana na magonjwa, kuhimili ukame na kuwa na mavuno mengi.

Bw. Seuri Mollel, mtafiti wa zao la mahindi, pamoja na Bw. Ismail Ngolinda, mtafiti mwandamizi wa mazao ya ngano na shayiri, wameeleza kuwa wakulima waliopokea teknolojia hizo wameweza kuboresha uzalishaji na kukabiliana na changamoto za kilimo katika mazingira yenye mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. Caresma Chuwa, pamoja na kuelezea malengo ya kituo katika kuwawezesha wakulima kulima kwa tija na kibiashara, amesema...


Kwa ujumla, wataalamu na watafiti wa kilimo kutoka TARI Seliani wameendelea kusisitiza kuwa mbegu bora zenye virutubisho ni suluhisho la kisayansi linaloweza kuchangia si tu kuongeza uzalishaji wa mazao, bali pia kupunguza mzigo wa magonjwa yanayotokana na lishe duni. Ni wakati wa wadau wote wa kilimo na afya kushirikiana kuhakikisha teknolojia hizi zinamfikia kila mkulima nchini.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...