Safiri Smart! Wataalamu kutoka sekta ya usafiri wakichambua njia za kufungua fursa za kidigitali nchini Tanzania kupitia ubunifu, sera thabiti na ushirikiano wa sekta mbalimbali ili kujenga mfumo wa usafiri jumuishi na endelevu

Ubunifu katika Misitu! Rais wa Finland, Alexander Stubb, akizindua mpango wa Green Catalyst unaolenga kuhamasisha ubunifu katika sekta ya misitu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania chini ya mradi wa ubunifu wa FUNGUO

Ushirikiano ni Muhimu! Mjadala wa Mawaziri kutoka Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji (Prof. Kitila Mkumbo), Elimu, Sayansi na Teknolojia (Prof. Adolf Mkenda) na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira, na Watu wenye Ulemavu (Mh. Patrobas Katambi) wakijadili mbinu za kuijenga Tanzania bora ijayo kwa kutumia ubunifu na teknolojia ya kisasa kama nguzo ya uchumi jumuishi na imara

Taifa la Leo! Vijana pia wakijadili changamoto na fursa zinazopatikana kupitia ubunifu, na namna wanavyoweza kuingia kwenye ulimwengu wa kidijitali na kujiajiri kwa kutumia suluhisho bunifu. 

Tupo Pamoja! Rais wa Finland, Alexander Stubb (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, wakiwemo Balozi wa Umoja wa Ulaya Ms. Christine Grau (wa kwanza kushoto), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Finland nchini, Ms. Theresa Zitting (wa tatu kutoka kushoto), Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Ndugu John Rutere (wa pili kutoka kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano na Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (wa kwanza kulia),  baada ya kuzindua mpango wa Green Catalyst kwa maendeleo ya sekta ya misitu nchini Tanzania

Fursa ya kipekee kwa vijana! Viongozi wa Rasilimali Watu kutoka katika mashirika na makampuni mbalimbali nchini Tanzania walikutana ana kwa ana na vijana walioko vyuoni bila kuwasahau wahitimu wa vyuo mbalimbali na kuwapa mbinu za kutafuta ajira, kuandika CV na jinsi ya kung’ara katika soko la ajira la sasa

Kujenga kizazi cha wanasayansi wa baadaye! Programu ya Code Like A Girl ya Vodacom Tanzania inawawezesha wasichana kupata ujuzi wa kufanya coding na kuongeza uwezo wao wa kujiendeleza katika sekta za ubunifu na teknolojia nchini
Ubunifu kwa Vitendo! Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Patrobas Katambi akiangalia drone ambayo inawasaidia wakulima mkoani Morogoro kufanya kilimo cha kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia ya kidijitali na hivyo kuongeza mapato yao

Usalama wa kidijitali ni msingi wa maendeleo. Athumani Mlinga, Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania, akizungumza na vijana wabunifu wakati wa zoezi mbashara la kufanya udukuzi salama katika mada ya ‘Ethical Hacking’
Baada ya wasilisho lake kuhusu matumizi sahihi na salama ya Akili Mnemba (AI), Mo Gawdat (kulia), gwiji wa kimataifa katika masuala ya AI, alipata fursa ya kuonesha baadhi ya vitabu vyake kwa washiriki katika mkutano huo. Pichani ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (kushoto) na Philip Basiimire, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...