Songea-Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura, amewapandisha vyeo askari 155 waliohitimu mafunzo ya upandishaji vyeo kwa mwaka 2024/2025 na kufaulu kwa mafanikio.

Shughuli ya uvalishwaji wa vyeo hivyo imefanyika katika viwanja vya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Ruvuma, na kuhudhuriwa na maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutoka vitengo tofauti vya jeshi hilo mkoani humo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kamanda Chilya amewataka askari waliopandishwa kuhakikisha wanavitendea haki vyeo walivyopokea kwa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu, weledi na kwa kuzingatia misingi ya haki, kama alivyoagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Aidha, aliwataka maafisa na askari wote kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha usalama wa wananchi na kuimarisha uhusiano bora kati ya Jeshi la Polisi na jamii, kupitia huduma zinazozingatia maadili na sheria.

Kabla ya kuanza kwa zoezi la uvalishwaji wa vyeo, Kamanda Chilya alikagua gwaride rasmi la heshima lililoandaliwa na askari hao, kisha kufanya mkutano mfupi wa baraza na kujadiliana nao masuala mbalimbali.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...