
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde akikabidhi hundi za malipo ya mrabaha kwa viongozi wa vijiji 5 vinavyozunguka mgodi wa Barrick North Mara malipo ya mrabaha katika hafla hiyo

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde akikabidhi hundi za malipo ya mrabaha kwa viongozi wa vijiji 5 vinavyozunguka mgodi wa Barrick North Mara malipo ya mrabaha katika hafla hiyo


Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde akikabidhi hundi za malipo ya mrabaha kwa viongozi wa vijiji 5 vinavyozunguka mgodi wa Barrick North Mara malipo ya mrabaha katika hafla hiyo


Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde akiongea katika hafla hiyo

Mbunge wa Tarime vijijini, Mhe. Mwita Waitara akiongea katika hafla hiyo

Meneja wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, akiongea katika hafla hiyo

Meneja wa Barrick Nchini, Dkt. Melkiory Ngido (Mwenye miwani katika mstari wa kwanza meza kuu) akiwa katika hafla hiyo
**
Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara, kwa mara nyingine umelipa malipo ya mrabaha kiasi cha shilingi bilioni 1.498 kwa vijiji vitano ilivyopo jirani na mgodi huo ikiwa ni malipo ya robo ya kwanza kwa mwaka wa 2025.
Hundi za malipo hayo kwa viongozi wa vijiji hivyo yamekabidhiwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde wakati wa hafla ya Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick kugawa leseni za kuchimba dhahabu kwa vikundi 48 vya vijana katika vijiji vinavyozunguka mgodi wa Dhahabu wa North Mara, iliyofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe katika mji mdogo wa Nyamongo, wilayani Tarime.
Vijiji ambavyo vimenufaika na mgao huo ni Nyangoto, Kerende, Nyamwaga, Genkuru na Kewanja na kila robo ya mwaka vimekuwa vikipokea gawio la malipo ya mrabaha kutokana na kuwa na haki ya kuchimba dhahabu katika shimo la Nyabigena (ambalo ni sehemu ya Mgodi wa Barrick North Mara) kabla ya kampuni ya Barrick kukabidhiwa kuendesha mgodi huo kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals kuanzia mwaka 2019.
Meneja Mkuu wa mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko,amesema kuwa malipo haya ni mwendelezo wa malipo ya mrabaha ambayo yamekuwa yakitolewa kwa vijiji hivyo kila kipindi cha robo mwaka kwa mujibu wa makubaliano na mgodi.
Waziri wa Madini,Mhe. Anthony Mavunde, ameipongeza Barrick North Mara kwa kuendelea kutoa gawio hilo la mrabaha ambalo linasaidia kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo katika vijiji hiyo ambavyo pia vinanufaika na fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zinazotolewa na mgodi huo katika wilaya ya Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla.
Nao Wenyeviti wa vijiji vilivyopata mrabaha wameshukuru na kuupongeza mgodi wa North Mara kwa jinsi unavyoendelea kusaidia jamii na kunufaisha vijiji vinavvouzunguka sambamba na kuimarisha uhusiano na jamii.
“Tunashukuru mgodi kwa kuendelea kutekeleza makubaliano sambamba na kusaidia kuchochea maendeleo katika maeneo yetu,”amesema Mwenyekiti wa kijiji cha Nyangoto,Zacharia Machange baada ya hafla hiyo wakati akiongea kwa niaba ya wanufaika.
Katika hatua nyingine Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick imegawa leseni za kuchimba dhahabu kwa vikundi 48 vya vijana katika vijiji vinavyozunguka mgodi wa Dhahabu wa North Mara .
Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde amezindua mradi huo wa utoaji leseni wa uchimbaji mdogo kwa vijana wakiwemo wanawake katika hafla hiyo.
Mh. Mavunde ameipongeza kampuni ya Barrick ambayo inaendesha Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa ubia na Serikali ya Tanzania kwa kutoa ushirikiano mkubwa ambao umesaidia kufanikisha utoaji wa leseni hizo.
“Napenda kuipongeza Barick North Mara kwa hatua hii nzuri. Tulizungumza tukaelewana kwa urahisi sana”, Waziri Mavunde amesema huku akiuita mradi huo kuwa wa kihistoria nchini Tanzania na wenye lengo la kuleta manufaa makubwa ya kiuchumi kwa vijana.
Alisema utoaji wa leseni hizo kwa vijana wa Nyamongo ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Mining for Brighter Tomorrow (MBT) akisisitiza kuwa lazima uwe na mafanikio yaliyokusudiwa.
“Zaidi ya vijana 2,000 wanaenda kunufaika na mradi huu , tutaupatia kipaumbele, ndio mradi wa kwanza mkubwa na wa kielelezo tutakaousimamia”, amefafanua Mavunde.
Amedokeza kuwa wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Dunia (WB) wameonyesha nia ya kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.“Benki ya Dunia, imevutiwa sana na mradi huu, vijana twendeni tukafanye kazi” ,amesema Waziri huyo wa Madini.
Wanufaika wa mradi huo walishukuru serikali ya awamu sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Hassan kwa kuwapatia leseni hizo.
“Uchimbaji wa madini una faida , tuna matarajio ya kuinua kipato chetu na tumefurahi sana na tunamshukuru Mhe. Rais wetu “,amesema Deborah Daniel Ryoba kutoka kikundi cha Nyabikondo Mining.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...