Benki ya Exim, kwa kushirikiana na mshirika wake wa kimataifa, MasterCard, imekabidhi rasmi zawadi kwa mshindi wa kampeni ya “UEFA Priceless”, Bi. Manjeet Kaur Mair, katika tukio maalum lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Bi. Mair alijishindia zawadi hiyo kupitia matumizi ya kadi ya Exim MasterCard (Debit), ambapo alifanya miamala mingi zaidi katika kipindi cha kampeni, na hivyo kuibuka kidedea. Mshindi huyo, pamoja na marafiki au ndugu watatu. atapata fursa ya kwenda kushuhudia mechi ya fainali za UEFA Champions League katika mbuga ya wanyama ya Amboseli nchini Kenya.

“Tunaendelea kuwatia moyo wateja wetu kutumia kadi zetu za Exim-iwe ni debit au credit-ili kujishindia zawadi mbalimbali katika kampeni zetu zijazo,” alisema Silas Matoi, Mkuu wa Huduma Mbadala za Kidigitali wa benki hiyo.

Mbali na zawadi hiyo, Exim Bank pia imetangaza kampeni nyingine mbili zinazotoa fursa kwa wateja wake kunufaika zaidi zikiwemo kampeni ya ununuzi wa tiketi za usafiri kwa ndege za Kenya Airways, ambapo mteja anapata zawadi ya tiketi zenye thamani ya hadi $315, na nyingine inayohusu ndege za Emirates, ambapo mteja anaweza kushinda tiketi zenye thamani ya hadi $2,000.

Mshindi wa kampeni hii Bi. Manjeet alisema, “Kutumia Exim Debit MasterCard kwa manunuzi ya mtandaoni na kimataifa kumefanya maisha yangu kuwa rahisi-ni huduma nzuri na isiyo na bughudha. Sasa ninasafiri na familia yangu kwenda Amboseli-kitu ambacho sikuwahi kufikiria kingetokea!”

Kwa kuendelea kutumia kadi za Exim MasterCard, wateja wanazidi kuwekwa kwenye nafasi ya kushiriki na kushinda katika promosheni za kipekee zinazozinduliwa mara kwa mara.

Mshindi kutoka Benki ya Exim Tanzania wa kampeni ya ‘UEFA Priceless’ Manjeet Kaur Mair (wa pili kutoka kushoto) akipongezwa na Silas Matoi (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kidijitali wa Benki ya Exim katika kampeni iliyolenga kuhamasisha matumizi ya Exim Mastercard ambapo mshindi anapata fursa ya yeye na marafiki ama ndugu watatu kwenda kushuhudia fainali za UEFA katika mbuga ya wanyama ya Amboseli nchini Kenya. Kushoto ni Meneja wa Akaunti ya Mastercard Tanzania, Moses Alphonce James na Kauthar D’souza (kulia), Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Exim wakati wa hafla hiyo iliyofanyika tarehe 21 Mei 2025 katika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.




Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...