Madaba_Ruvuma.

Tarehe 21 Mei 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Ndugu Sajidu Idrisa Mohamed, amefanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Madaba kwa lengo la kujionea maendeleo na maboresho makubwa ya huduma za afya yanayoendelea kutekelezwa hospitalini hapo.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi alipata fursa ya kupokea huduma ya matibabu kutoka kwa wataalamu wa afya waliopo hospitalini, jambo linalothibitisha imani na kuridhishwa kwake na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Akizungumza na watumishi pamoja na wananchi waliokuwepo hospitalini, Mkurugenzi aliwahimiza kutumia kikamilifu huduma zote zinazopatikana katika Hospitali ya Wilaya ya Madaba. Alisisitiza kuwa huduma nyingi ambazo awali zililazimu wananchi kusafiri nje ya halmashauri sasa zinapatikana ndani ya hospitali hiyo.

Aidha, alitangaza kuwa kuanzia tarehe 26 hadi 31 Mei 2025, kutakuwa na kambi maalum ya madaktari bingwa na mabingwa bobezi itakayofanyika hospitalini hapo. Kambi hiyo itaendeshwa kupitia mpango maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi aliwaalika wananchi wote wa Wilaya ya Madaba na maeneo jirani kufika kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa zitatolewa kwa gharama nafuu, akisisitiza kuwa ni fursa ya kipekee inayopaswa kutumiwa ipasavyo kwa ajili ya kuboresha afya za wananchi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...