Wajumbe wa Bodi ya VETA (VETA BOARD) imeutaka uongozi wa VETA kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi ya kufundishia ili iwe kimbilio kwa kila mmoja huku ikisisitiza VETA ni kwa ajili ya wote.

Agizo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Clotilda Ndezi wakati wa ziara ya bodi hiyo katika Chuo cha VETA Shinyanga ambapo walitembelea kujionea hali ya utoaji wa mafunzo katika chuo hicho.

Makamu Mwenyekiti huyo amesema VETA sio ya waliofeli ila ni kwa wote waliomaliza masomo katika kada mbalimbali na watu mbalimbali wanaweza kwenda kwa ajili ya kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kuweza kujipatia kipato.

“VETA imejikita haswa kutekeleza agizo la serikali kwa vijana kuweza kujiajiri na kuweza kuwa makamupini yao. Wito kuwaita watanzania waliokaribu na vituo vya veta waweze kutumia fursa bila hofu Veta imejipanga kuweka mazingira wezeshi,”amesema Makamu Mwenyekiti huyo, na kuongeza

“Tunaposema ni kwa ajili ya wote ni lazima vitu vya msingi tuvitafakari inamaana kwamba hata mimi niweze kuja VETA, Mama aliyeko nyumbani aseme ngoja niende VETA nikajifunze mwingine aseme nahitaji mafundi bomba tunapotazama ramani ya namna hiyo tunatakiwa kuwa na mitazamo ya ziada tuongeze kufikiria zaidi.Mazigira tunayajenga kiasi gani ili wajisikie kwamba wapo mahali sahihi,”amesema Bi.Ndezi

Amesema ziara yao kama wajumbe wa bodi Mkoani Shinyanga wamezeza kujionea kwa jinsi ambavyo vijana wanapata ujuzi katika umeme kungarisha vito urembo kuendesha mitambo makubwa na fani zingine nyingi Kuhusu ziara amesema kuwa lengo lilikuwa ni kuona namna ya kuboresha zaidi undeshaji wa vyuo ili kuendana na teknolojia ambapo amedai kunatakiwa kuwa na mitambo ya kisasa ambayo itasaidia kwendana na teknolojia. “Kuna umuhimu wa kushirikiana na makampuni ili kuona mahitaji yao cha kufurajisha kuna wanafunzi kutoka Nchi za jirani mafunzo haya ni ufundi haswa kwa kuweza kumjerngea kesho mtu yoyoye,”amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi VETA Kanda ya Magharibi,Asanterabi Kanza amesema kuwa wamefarijika kuona wajumbe wa bodi kwenda kujionea shughuli zinavyoendelea ambapo wameonekana kuvutiwa na vitu mbalimbali “Wamejionea jinsi ambavyo wanafunzi wanaendesha mitambo na fani mbalimbali na wametoa maelekezo na tunashukuru wameweza kuzungumza na wafanya nimefarijika wamezungumza na wafanyakazi wameweza kusikia kwa wale wanaosimamia mamlaka hizi,”amesema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...