WAFANYABIASHARA wa Ubungo hususan wanaofanya biashara zao katika maeneo ya Goba na madale wametakiwa kufuata sheria kwa kurasimisha biashara zao kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kukadiriwa na kulipa kodi stahiki.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Mkwawa ametoa wito huo leo Mei 21, 2025kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando alipokutana timu ya maafisa wa Mamlaka hiyo ikiongozwa na Meneja wa TRA mkoa wa kikodi Tegeta Dickson Qamara

Mkwawa amesema, kuna biashara nyingi mpya zinazoanzishwa katika eneo la Goba na baadhi ya wafanyabiashara bado hawajazirasimisha biashara zao hivyo amewataka kufuata sheria kwa kurasimisha biashara hizo serikalini ili waweze kulipa kodi inayostahili.

"Ninawakumbusha wafanyabiashara kutii sheria za kikodi...kweli kumekua na changamoto hasa haya maeneo ambayo yameibuka kuwa na biashara nyingi, kuna idadi ndogo ya watu kwenda kurasimisha biashara zao na kukadiriwa ili waanze kulipa kodi"

Ameongezea kwa kuwakumbusha wafanyabiashara hao kuendelea kutumia mashine za EFD kutolea risiti kwani matumizi ya mashine hizo ndio msingi wa watu kulipa kodi halali kwa sababu mashine hiyo inauwoweza wa kuonyesha mauzo yake yote aliyoyatolea risiti.

"Mashine ya EFD ni msingi wa watu kulipa kodi halali hasa anachopaswa kulipa kwa sababu Mashine hiyo ndio inaonyesha taarifa zake zote jinsi mauzo yake yalivyo..."

Amesema anafahamu kuwa kuna baadhi ya changamoto ambazo wafanyabiashara wanakumbana nazo kwa kiasi kikubwa ikiwemo kukosa elimu sahihi ya kodi hivyo watumia fursa ya zoezi la elimu ya kodi ya mlango kwa mlango kupata kujua mambo mbalimbali ya kodi.

Kwa upandewake, Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka TRA mkoa wa Kikodi Tegeta, Mercy Macha amesema katika zoezi hilo liloanza Mei 19, .2025 wamebaini kuwa kuna wafanyabiashara wengi wapya na baadhi yao wa zamani bado hawajakadiriwa hivyo amewashauri wafike katika ofisi za TRA zilizopo karibu kwa ajili ya kukadiriwa na kufanya malipo ya kodi zao.

Nae, Noela Mushi mmoja wa wafanyabiashara wa eneo la Goba ameishukuru TRA kwa kuwatembelea na kuwaelimisha juu ya mambo mbalimbali ya kodi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Mkwawa (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa TRA Mkoa wa Kikodi kikodi wa Tegeta, Dickson Qamara  wakati timu ya Maafisa wa TRA walipotembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara maarufu kama mlango kwa mlango
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Hassan Mkwawa (kushoto) akizungunza na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati timu ya Maafisa hao walipotembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo  kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara, maarufu kama mlango kwa mlango.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...