•CCM inaheshimu ushauri wa Jaji Warioba ila bahati mbaya CCM ina mahusiano mazuri na CHADEMA
•Wamuomba awe msuluhishi wa Mgogoro ndani ya CHADEMA na CCM itatoa mchango
MOROGORO: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakina migogoro na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwani wanahusiana vizuri na chama hicho na kwenye chama cha vyama vya siasa (TCD) wanashiriki vizuri na mwenyekiti anatoka CHADEMA
CCM imesema imepokea ushauri uliotolewa na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba kwani wanaheshimu ushauri unaotolewa naye, lakini hakuna tofauti wala migogoro iliyopo kati ya CCM na Chadema na iwapo itatokea watatumia ushauri huo kufanya suluhu.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameeleza hayo leo Mei 5,2025 wakati akizungumza na wananchi wa eneo la Mikese katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku saba katika mkoa huo.
Jaji Warioba akiwa katika Kongamano la Uchaguzi Mkuu lililoandaliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa siasa, vikiwemo vyama vya siasa alishauri serikali kukaa katika meza ya mazungumzo na Chadema pamoja na CCM.
Lengo likiwa ni kupata kupata muafaka wa amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Akijibu hilo Makalla amesema Mzee warioba ni mbobevu katika mambo ya uongozi na mwanasheria nguli ambaye anamchango mkubwa katika taifa hili na ushuri wake unaheshimika sana na wataendelea kuheshimu michago ya wazee wa taifa pale wanaposhauri.
“Tutaendelea kuheshimu michango yao wanapotushauri, akasema CCM tumalize mgogoro wa kisiasa mimi nataka niseme ushauri wake tumeupokea lakini hauwezi ukatumika sasa kwa sababu CCM haina mgogo wa kisiasa na Chadema,” amesema Makalla.
Ameongeza: “Ushauri wake unaweza kuja kutumika pale itapokuja kutokea Mgogoro ila sisi na Chadema hatuna mgogoro na tuna mahusiano mazuri na Chadema . Tuna CDD na mwenyekiti wa Chadema ndiye anakuwa mwenyekiti wa TCD ambacho ni kituo cha demokrasia kinachohusisha kinachohusisha vya vyote vya siasa Huko ndiyo Tuma kuongea mambo yetu ya siasa
Katika hatua nyingine Makalla ameomba ushauri huo uliotolewa ukatumike na akawe msuluhishi wa mgogoro uliopo ndani ya Chadema awaite G-55 na wakae wamalize mgogoro wao na CCM wapo tayari kushiriki na kuchangia mazungumzo hayo ili waweze kusuluhisha.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...