•kutangaza kuhama kwa waliokua viongozi waandamizi ni uthibitisho mgogoro ndani ya Chadema

MVOMERO: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawakaribisha kujiunga na chama hicho John Mrema na wenzake kutoka katika kundi la G55 waliojiondoa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameeleza hayo leo Mei 7,2025 wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku saba katika mkoa huo.

Makalla ameeleza hayo baada ya wajumbe wa Sekretarieti ya Chadema iliyomaliza muda wake akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge na Mrema kutangaza kujiondoa katika chama hicho kuanzia leo.

Makalla amebainisha kuwa amefurahishwa na kauli ya G55 kwamba walihitaji kuondoka Chadema kwa sababu wanachama hao ndoto na haja yao ni kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Ameongeza pamoja na kundi hilo hawajaweka wazi ni chama gani ambacho wanania ya kwenda kujiunga nacho kati ya vyama 18 vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi, lakini Makalla alisema wanawakaribisha kuwa wanachama wapya wa CCM kwani wao wapo tayari kushiriki uchaguzi.

“Pamoja na kuondoka Chadema G-55 hamjaeleza chama mnachoenda sisi CCM tunawakaribisha milango iko wazi jiungeni na Chama cha Mapinduzi, vyama 18 vimeamua kushiriki uchaguzi kasoro chama kimoja,”amesema Makalla.

Ameongeza: “kwahiyo katika vyama 18 mnaweza kuangalia vyamba mbalimbali lakini mimi kama msemaji wa chama nawakaribisha CCM twende kwenye uchaguzi tushinde kwa kishindo”.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...