Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mhe. Mkali Kanuso, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon kwa utawala bora ambao umechangia kuwepo kwa utulivu na maendeleo Wilayani humo.

Akizungumza leo Mei 7, 2025, wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kujadili taarifa za maendeleo kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025, Mhe. Kanuso alisema kuwa uongozi wa Nickson umejikita katika haki, usikivu, na uwajibikaji wa hali ya juu.

“Nickson anafanya vizuri sana; ni kiongozi mpole, msikivu, mtulivu, mchapa kazi na mpenda haki. Tunajivunia kuwa naye hapa Kibaha na tunamuomba Mheshimiwa Rais aendelee kumbakisha hapa ili tuendelee kufaidika na uongozi wake,” alisema Kanuso.

Pia, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha alitoa pongezi kwa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kwa kufanikisha kupungua kwa kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 4.1 hadi asilimia 3.4. Pongezi hizo zilienda sambamba na utoaji wa vyeti vya pongezi kwa wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa CHADEMA Kibaha Vijijini, Mhe. Weston Sinkonde, alilipongeza Baraza la Madiwani kwa kazi nzuri wanayoifanya, na kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa ushirikiano wa karibu na vyama vya upinzani.

“Kibaha Vijijini tumebahatika kupata Mkurugenzi wa aina hii. Amejitoa, anatufikia na kutusikiliza bila ubaguzi. Hakika huyu ni zawadi kutoka kwa Mungu,” alisema Sinkonde.

Awali, wakati wa uwasilishaji wa taarifa za Kamati ya Uchumi na Mazingira, Mhe. Rehema Kibwana alimsifu Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usafi wa Mazingira, Maximilian Ntobu, kwa kuifanya Mlandizi kuwa moja ya maeneo safi kwa juhudi kubwa za yeye na wasaidizi wake.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...