Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
SERIKALI imetoa vifaa vya kisasa vya utafiti wa maji chini ya ardhi,huku ikitoa maagizo kwa mamlaka za maji kuhakikisha zinafanya tafiti za kina ili kuhakikisha watanzania wote wanapata maji.
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma katika hafla ya makabiadhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.2,kwa mabonde nane ya Maji hapa nchini.
Aweso amesema vifaa hivyo vya kisasa ambavyo vimenunuliwa kwa za fedha za Uviko 19,vinakwenda kumaliza changamoto ya maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambayo bado hayajafikiwa na maji kwa asilimia inayotakiwa.
Kutokana na hilo,ameziagiza mamlaka hizo kuhakikisha vijiji zaidi ya 1,500 ambavyo vilikuwa havina maji kuhakikisha vyote vinapata maji ili kutimiza azma ya Serikali ya kumtua ndoo mama kichwani.
"Sasa hivi natarajia kutosikia kikwazo chochote kutoka kwa wataalam wa sekta za maji kuhusu upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali hususani vijijini na baadhi ya maeneo mjini kafanyeni tafiti za kina kupitia vifaa hivi,serikali imetoa vifaa vya kisasa ambavyo vinafanya utafiti umbali mrefu kwenda chini hivyo maji yatapatukana,"alisema Aweso.
"Kuna baadhi ya maeneo walikuwa wanasema hakuna maji,ukienda wakielekezwa maji yanapatikana,natumaini hivi sasa hakutakuwa na malalamiko hayo,"alisema.Aweso.
Alifafanua zaidi ya kuwa na hii yote ilitokana na ukosefu wa vifaa vya kisasa lakini hivi sasa natumaini changamoto zote hizo kwa wataalamu kwenye kupata takwimu za maji chini ya ardhi hazitakuwepo.
Naye Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Dkt George Lugomela amesema vifaa hivyo vitatumika kuchunguza mipasuko kwenye matabaka ya miamba inayoweza kuhifadhi maji,kuchunguza uwepo wa maji kwenye.matabaka ya miamba.
Vifaa hivyo pia vitawasaidia wataalam wa sekta ya maji kupima uwepo wa maji kwa njia tatu lakini pia kina uwezo wa kwenda kuchunguza maji umbali wa mita 1,000,huku vifaa vingine vikitumika kupima kina cha maji kwenye visima virefu.
Aliongeza kusema pia baadhi ya vifaa vingine vitatumika kuchunguza mikondo ya maji na aina ya matabaka ya miamba,huku kifaa kingine kitatumika kuchukua majira ya nukta kwenye visima ili kuingizwa kwenye ramani.
Alivitaja vifaa hivyo vilivyonunuliwa ni pamoja Magnetometer Tisa,Tetrameter tisa,Deeper tisa,Borehole Logger, na Accessories.
Aliyataja pia mabonde ambayo yamekabidhiwa vifaa hivyo ni pamoja na Tanganyika,Victoria,Wami -Ruvu,Rukwa Ruvuma,Rufiji,Pangani na Bonde la Kati,huku vifaa vingine vitabakia makao Makuu.
Awali akimkaribisha Waziri,Katibu Mkuu wa Wizara Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,aliishkuru Serikali huku akisisitiza hivi sasa kazi za maji zinakwenda kufanyika kwa weredi mkubwa kutokana na uwepo wa vifaa hivyo vya kisasa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...