Farida Mangube, Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, ameutaka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kuhakikisha unaandaa mitaala ya kisasa itakayowajengea vijana ujuzi unaokidhi mahitaji katika sekta ya uvuvi na ufugaji wa viumbe maji.
Akizungumza mkoani Morogoro wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha siku 10 cha kupitia na kuhuisha mitaala 12 ya FETA, Prof. Shemdoe alisema mitaala hiyo inapaswa kuelekeza nguvu katika maeneo ya teknolojia ya kisasa, ufugaji wa viumbe wa majini, usindikaji na uhifadhi wa samaki.
"Ni muhimu mitaala hii izingatie pia mafunzo kwa vitendo, ili kuhakikisha kuwa wahitimu wanapomaliza masomo yao wawe na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa," alisema Prof. Shemdoe.
Aidha Prof. Shemdoe alisisitiza umuhimu wa mitaala hiyo kushughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi, akieleza kuwa vijana wanapaswa kufundishwa mbinu endelevu na rafiki kwa mazingira za uvuvi ili kupunguza athari katika sekta ya viumbe maji.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa FETA, Dkt. Semvua Mzighani, alisema lengo la kikao kazi hicho ni kupitia na kuhuisha mitaala mitano ambayo imepitwa na wakati, kutokana na mabadiliko ya sayansi, teknolojia, tabianchi, mahitaji ya ajira na sera mbalimbali za kitaifa.
"Mbali na kuhuisha mitaala mitano, tumeona kuna uhitaji wa mitaala mipya kumi na miwili itakayogusa sekta za uvuvi na utunzaji wa viumbe maji, hivyo jumla ya mitaala itakayofanyiwa kazi ni 17," alisema Dkt. Mzighani.
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bi. Rehema Nadhani, alisema ana matumaini kuwa kupitia mafunzo hayo, vijana watapata maarifa yatakayowasaidia kuleta mageuzi chanya katika sekta ya uvuvi na kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya kisasa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...