NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya elimu ameamu kutumia kiwango cha asilimia 85 za fedha za mfuko wa maendeleo ya Jimbo lake katika kuboresha na kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi ikiwa pamoja na kuweka miondombinu rafiki kwa shule zilizopo pembezoni mwa mji.
Koka ameyabainisha hayo wakati wa ziara ya kikazi ambayo ameambatana na wajumbe wa kamati ya mfuko wa jimbo kwa lengo la kuweza kutembelea na kugagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo ambayo baadhi yake inatekelezwa kupitia fedha ambazo zinaotokana na mfuko wa Jimbo.
Katika ziara hiyo wajumbe wameweza kupata fursa ya kutembelea katika shule ya msingi Misugusugu kwa lengo la kuweza kugagua utendaji wa kazi ya mashine kwa kunakili nakala za karatasi (Photocopy shine ) ambayo imegharimu kiasi cha shilingi milioni 4.5 pamoja na kutembelea mradi wa jengo la ofisi ya mtaa wa Miembesaba 'B'.
Aidha katika ziara hiyo Mbunge Koka na kamati hiyo wameweza kutembelea mradi wa ujenzi wa mradi wa kalavati mtaa wa mpakani kata ya Mkuza ambapo limeweza kukamilika na kuwa mkombozi mkubwa kwa kuwasaidia wananchi wa aeneo hilo kuweza kupita kwa urahisi hasa katika kioindi cha mvua.
"Ndugu zangu kwanza kabisa nipende kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Rais wetu wa awamu ya sita Dkt. kwa kuweza kutenga fedha nyingi katika Jimbo la Kibaha mjini ambazo zieweza kwenda kuwa ni mkombozi mkubwa katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo na kutatua kero na changamoto za wananchi,"amebainisha Mbunge Koka
Kadhalika katika ziara hiyo ya wajumbe hao wamewweza kupata fursa ya kukagagua mradi wa ujenzi wa maboma ya madarasa mawili katika shule ya msingi boko Timiza ikiwemo sambamba na kutembelea utengenezaji wa vitanda vya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Kibaha lengo ikiwa ni kuboresha sekta ya elimu.
Diwani wa Kata ya Misugusugu Upendo Ngonyani amemshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuweza kupambana kwa hali na mali kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kuwasogezea huduma mbali mbali za kijamii wananchi na kupelekea kupunguza kwa kiais kikubwa changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kongowe Hamis Shomari hakusita kumpongeza kwa dhati Mbunge Koka kwa kuweza kuwa mstari wa mbele katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa fedha za mfuko wa Jimbo ambazo zimeweza kwenda kusaidia kwa kiais kikubwa katika suala zima la kuboresha miundombinu ya majengo ya madarasa na kuchangia madawati na kufanya wanafunzi kuondokana na adha ya kukaa chini.
Ziara ya wajumbe wa kamati ya mfuko wa maendeleo ya Jimbo la Kibaha imeweza kufanya ziara hiyo ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika kata ya Misugusugu, Kongowe, Kibaha, Tumbi, pamoja na kata ya Mkuza katika sekta za elimu, miundombinu ya barabara, mradi wa ujenzi wa ofisi ya serikali pamoja na huduma za kijamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...