Benki Kuu katika ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) zimehimizwa kuweka kipaumbele katika kutumia rasilimali zao kwa ajili ya maendeleo yao, na kupunguza utegemezi kutoka nje.
Wito huo umetolewa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Mkutano wa 28 wa Kamati ya Masuala ya Fedha (MAC) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Mombasa, Kenya.
Amesema nchi wanachama wa jumuiya hii zimebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi zinazofaa kutumiwa kwa maendeleo ya kanda hii. Ameeleza kuwa licha ya maendeleo ambayo yamepatikana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, ukanda wa Afrika Mashariki unaendeleo kupitia changamoto nyingi za kiuchumi.
“Kumekuwa na kuongezeka kwa ushuru katika biashara, migogoro ya kimataifa na athari zinazotokana na tabianchi ambavyo vinahatarisha utulivu wa kiuchumi na jitihada za mtangamo,” amesema Gavana Tutuba.
Aidha, ametaja kukua kwa huduma bunifu za kifedha (fintechs) na fedha za kidigitali (cryptocurrencies), kama maeneo ambayo licha ya kuweza kuchangia kukua na ufanisi wa ujumuishi wa kifedha, yanaleta changamoto za usimamizi na uhalifu wa kimtandao.
“Hivyo, ushirikiano wa pamoja katika kuhakikisha uthabiti wa kifedha pamoja na kusaidia ukuaji wa endelevu wa kiuchumi ni muhimu. Lazima tushirikishane njia bora za utendaji, data, na uzoefu kwa jinsi tunavyofanya kazi pamoja na kujenga mazingira bora kwa kuchangia kukuza uchumi, ubunifu na uthabiti kikanda,"alisema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho, Magavana na wawakilishi kutoka Burundi, Rwanda, Somalia, Kenya, Sudani ya Kusini, Tanzania na Uganda, walielezea maendeleo ya kiuchumi ya nchi zao, pamoja na utayari wao wa kuhakikisha masuala ya mtangamano katika sekta kifedha yanafanikiwa.
Mkutano huo, ulioanza Jumatano na kamati ya wataalamu, umehitimishwa leo na magavana chini ya uenyekiti wa Gavana wa Benki Kuu ya Kenya, Dkt. Kamau Thugge. Aidha, viongozi hao wa benki kuu walitia saini taarifa ya pamoja ya mkutano huo inayoelezea yale yaliyojadiliwa na kukubaliwa katika mkutano huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...