Kukamilika kwa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Seronera (Seronera Airstrip) uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti umeelezwa kuwa kichocheo muhimu cha ongezeko la idadi ya watalii nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hassan Abbasi ameeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Seronera (Seronera Airstrip) uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti utachochea ongezeko la watalii wa ndani na nje.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Mei 9, 2025 wakati akifanya ukaguzi wa miundombinu ya utalii iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Aidha, Dkt. Abbasi alielekeza usimamizi wa uwanja huo baada ya kupokea maelezo ya kukamilika kwa ukarabati wa uwanja ambapo matengenezo yaliyofanyika ni pamoja na upanuzi wa eneo la uwanja lijulikanalo kana “Taxway”, njia ya ndege yenye urefu wa mita 15 pamoja na upanuzi wa sehemu ya kutua ndege (runway) yenye urefu wa Kilomita 2.3 na upana wa mita 30.

Ziara ya Dkt. Abbasi ni mwendelezo wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ambapo awali alitembelea na kukagua maeneo ya uwekezaji wa malazi katika hoteli ya Serengeti Explorer na Serengeti Lake Magadi Lodge zilizopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Dkt. Abbasi amewaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya utalii ikiwemo malazi katika Hifadhi ya Taifa Serengeti, hifadhi nyingine za Taifa pamoja na maeneo mengine yaliyohifadhiwa ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuhakikisha kuwa Tanzania inapokea idadi kubwa ya watalii na mapato yatokanayo na utalii.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...