Songea – Ruvuma
Wananchi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kupeleka fedha zilizochakaa, kuchanika au kuharibika katika benki yoyote iliyo karibu nao, kwani huduma ya kubadilisha fedha hizo hutolewa kwa mtu yeyote bila kuhitajika kuwa na akaunti ya benki husika.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) – Kanda ya Mtwara, Bw. Melchiades Domino Rutayebesibwa, wakati akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, katika mkutano wa utoaji elimu kuhusu utambuzi wa noti bandia.
Bw. Rutayebesibwa amesema kuwa ni haki ya kila Mtanzania kupata huduma hiyo kutoka benki yoyote ya biashara nchini, na kwamba wananchi hawapaswi kuhifadhi fedha zilizochakaa majumbani au kuacha kuzitumia kwa hofu ya kukataliwa, kwani benki zipo tayari kusaidia mchakato wa kubadilisha noti hizo.
Aidha, amewataka wananchi kuwa makini zaidi katika kipindi hiki cha mavuno kwa kutumia njia salama za malipo kama mitandao ya simu au benki, badala ya kubeba fedha taslimu mikononi, ili kuepuka hatari ya kulipwa noti bandia.
“Kwa mwaka huu 2025 hatujapokea taarifa rasmi ya uwepo wa noti bandia, lakini tahadhari ni muhimu wakati wote. Tunawahimiza wananchi kutumia njia za kielektroniki kama miamala ya simu katika shughuli za mauzo ya mazao, ili kuhakikisha usalama wa fedha zao,” alisema.
Katika elimu hiyo ya fedha, amewataka wananchi kujifunza namna ya kutambua noti halali kwa kutumia alama mbalimbali za usalama zilizopo kwenye fedha halali za Tanzania, sambamba na kuelewa wajibu wao katika kulinda thamani ya noti ya Taifa.
BoT inaendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya kifedha ili kuwawezesha Watanzania kufanya maamuzi sahihi na salama katika matumizi ya fedha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...