Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana kampuni ya Jolly Features wameandaa mafunzo kwa walimu wa shule ya msingi kuhusu mbinu za kufundisha Kiingereza ili kuwajengea umahiri utaosaidia wanafunzi kujifunza vyema.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza Mei 22, 2025 , huku yakihusisha walimu wa Darasa la Kwanza, katika kituo cha Isimba kilichopo halmashauri ya Nzega Mkoani Tabora.
Mratibu wa mafunzo katika Halimashauri ya Wilaya ya Nzega, Bw. Joshua Samson, amesema kuwa, walimu wanaoshiriki mafunzo wamepatiwa mbinu mpya mbalimbali za kufundisha lugha ya Kiingereza kwa wanafunzi wa Darasa la kwanza.
"Tunaishukuru Serikali kwa mafunzo haya, kwani mbinu mpya walizopewa walimu zitasaidia sana katika eneo la fundishaji kwa wanafunzi." Alisema Bw. Samson.
Aidha, Bw. Samson amesema, walimu kwa pamoja wanajifunza mbinu mbalimbali za ufundishaji Kiingereza zenye kuwajengea ujuzi wa kutumia mbinu ya Jolly Phonics kukuza stadi za Kusoma na Kuandika (Literacy Skills) kwa Kiingereza kwa wanafunzi wa ngazi husika.
Wakizungumza katika mafunzo hayo, walimu walioshiriki wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh.Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mafunzo kwa walimu, wakieleza kuwa yamewasaidia sana katika kuboresha ufundishaji wao watakaporejea katika vituo vya kazi.
Mafunzo hayo ni endelevu na yanafanyika nchi nzima, pia ni mahsusi kwa shule zinazotumia Kiswahili kufundishia kwa kuwa katika Mtaala ulioboreshwa lugha ya Kiingereza inaanza kufundishwa kuanzia Darasa la Kwanza katika shule hizo tofauti na zamani ambapo Kiingereza kilikuwa kinaanza kufundishwa Darasa la Tatu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...