Dodoma.

Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara (Samia Infrastructure Bond) inaenda kuondoa changamoto ya kutokamilika kwa wakati kwa ujenzi na matengenezo ya miundumbinu ya barabara kutokana na ucheleweshaji wa malipo kwa makandarasi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA), Bi. Catherine Sungura wakati akijibu katika kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Alisema katika bondi hiyo, TARURA kwa kushirikiana na Benki ya CRDB imefanikiwa kukusanya bilioni 323 ambazo zitaenda kutumika kuwakopesha Makandarasi wazawa ili waweze kukamilisha ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Bi. Sungura alisema TARURA itaendelea kushirikiana na maafisa habari kwenye Halmashauri katika kutangaza kazi kubwa ya ujenzi na matengenezo ya miundumbinu ya barabara nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...