Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
JAMII imehaswa kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara afya ya moyo ikiwa ni hatua muhimu ya kugundua magonjwa mapema na kupunguza gharama za matibabu.
Wito huo umetolewa leo Mei 21,2025 na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Appolinary Kamuhabwa wakati akizindua rasmi kambi ya upimaji bure wa magonjwa ya moyo itakayodumi kwa siku mbili mfululizo katika Kampasi ya Mloganzila.
Amesema kambi hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa kukabiliana na ongezeko la magonjwa ya moyo na inahesabiwa kama moja ya shughuli muhimu kuelekea uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Huduma za Moyo.
“Uchunguzi wa mapema unaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za matibabu na, muhimu zaidi, kuokoa maisha ya watu wengi.Kambi hii inakuja wakati ambao takwimu za magonjwa ya moyo Afrika Mashariki zinaongezeka. Kituo cha Umahiri ni jibu muafaka na la kimkakati katika kukabiliana na janga hili la kiafya,"amesema Profesa Kamuhabwa
Ameongeza,"Kituo hiki kikianza kazi rasmi kitabadili kabisa namna ya kutibu magonjwa ya moyo nchini Tanzania pamoja na ukanda mzima wa Afrika Mashariki,"
Ikumbukwe kuwa,MUHAS inatoa programu maalumu 93 za kitaaluma, zikiwemo Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Tiba inayopokea wanafunzi 20 kwa mwaka, pamoja na programu za Tiba ya Moyo kwa Watoto na Misingi ya Moyo, kila moja ikiwa na udahili wa wanafunzi 10 kwa mwaka.
Aidha,chuo kinapanga kupanua mitaala yake kwa kuanzisha programu mpya katika upasuaji wa moyo, ganzi na uuguzi, ili kukidhi mahitaji ya huduma za afya katika kanda.
Naye Makamu Mkuu wa MUHAS anayeshughulikia Taaluma, Profesa Emmanuel Balandya ameeleza kuwa huduma za chuo zinafikia mataifa jirani na ni asilimia 10 ya wagonjwa wanaohudumiwa katika vituo vya afya vya MUHAS wanatoka nje ya Tanzania.
“Hii inaonyesha kuwa mahitaji ya huduma maalum za kiafya yanazidi kuongezeka katika ukanda huu na ili kutimiza malengo yetu ya kitaaluma na huduma za tiba, MUHAS inawekeza kwa kiasi kikubwa katika vifaa vya kisasa vya utafiti na ufundishaji. Pia maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kuanzisha huduma kamili za fiziolojia,"amesema Balandya.
Amesema kupitia mkakati huo wa kisasa, MUHAS inaonyesha wazi kinga, elimu kwa umma, na suluhisho za kiafya zenye ubunifu zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya maelfu ya watu katika miaka ijayo.
Mkazi wa Mahunguchira, Mbagala,Wilaya ya Temeke, Mtemi Chitema amesema huduma hiyo itasaidia kuimarisha afya za jamii na kutoa wito wa kupeleka huduma hizo vijijini ilikunusuru wagonjwa wasiojiweza.
“Hii ni huduma ya thamani inayopaswa kudumishwa na kupanuliwa zaidi, kupitia Vituo vya afya vya wilaya vinapaswa kutoa huduma za kudumu za uchunguzi wa moyo ili kuongeza upatikanaji wa vipimo vya mara kwa mara pale mtu anapohisi utofauti wa Afya yake,"amesema Chitema
Naye mkazi wa Mbezi,Maria Thadeus amewapongeza watumishi wa afya waliotoa huduma hiyo, akisema wameonyesha weledi na huduma bora wakati wote wa kambi hiyo
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), magonjwa ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo duniani, ambapo 2019 pekee, yalichangia vifo vya watu takribani milioni 17.9 sawa na asilimia 32 ya vifo vyote.

Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa akizungumza leo Mei 21, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kambi ya siku mbili ya uchunguzi wa afya ya moyo iliyofanyika kaika Kampasi ya Mloganzila, Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu,

Wananchi kutoka maeneo mbali mbali nchini wakipatiwa elimu ya namna ya kujilinda na magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa Moyo wakati wa ufunguzi wa kambi ya siku mbili ya uchunguzi wa afya ya moyo iliyofanyika kaika Kampasi ya Mloganzila, Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu leo Mei 21,2025

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini wakipata huduma ya uchunguzi wa afya ya moyo katika Kampasi ya Mloganzila, Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma MUHAS , Prof. Emmanuel Balandya akizungumza wakati wa ufunguzi wa kambi ya siku mbili ya uchunguzi wa afya ya moyo ilifanyika katika Kampasi ya Mloganzila, Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...