Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh Mohammed Mchengerwa amewataka Maafisa Habari wa Mikoa,Halmashauri na Taasisi zote zilizopo chini ya Ofisi yake kuendelea kuandaa mpango kazi kulingana na vipaumbele vya Taasisi au Mamlaka ambavyo vitasaidia kwenda kuelemisha jamii na Taifa kwa ujumla.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 23,2025 Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa ,Halmashauri na Taasisi zote za Ofisi ya Rais -TAMISEMI.
Sambamba na kuwataka Maafisa hao kuwa wabunifu kati uchakati wa habari,kuandika na kusambaza ili ziweze kuwafikia Watanzania sambamba na kuwa wazalendo kwa kuandika habari za kuelimisha,kufundisha na zenye tija kwa jamii nzima.
"Maagizo yangu kwenu Maafisa Habari, kwanza kila mmoja atambue kuwa hakuna haki bila wajibu,hivyo nawaelekeza kuwa kila Afisa Habari aendelee kuandaa mpango kazi kutokana na mpango mkakati wa Taasisi aua Mamlaka husika na vipaumbele vya Taasisi au Mamlaka ambavyo kwa ujumla vitasaidia kwenda kuelimisha jamii".
Aidha Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo kwa Makatibu tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka zote za Serikali za Mitaa kupitia Katibu Mkuu kuhakikisha kuwa Maafisa habari hao wanashiriki kikamilifu katika ziara zote za Viongozi pamoja timu za tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo kwa lengo la kuwezesha kuwa na uelewa na kazi zinazofanywa na Mikoa na Halmashauri ili kuweza kuujulisha Umma mambo yanayofanywa na Serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa Tanzania amesema kwa sasa changamoto moja waliyonayo ni ile ya kuhakikisha kundi gani linapata habari gani,badala ya kuandika habari moja ambayo haitafurahiwa na watu wote.
Hivyo kila kundi linatakiwa liwe na aina yake ya habari ya kulifikia kundi husika ili Watanzania wote wajue lengo la habari na hasa wakati ambao wanakuwa na jambo muhimu la kuwafikia Watanzania.
Mafunzo haya yamewakuatanisha Maafisa kutoka Mikoa na Halmashauri zote Nchini yenye lengo la kufanya tathmini kwa pamoja ya utendaji wa kazi katika maeneo yote pia kubadilishana uzoefu nankujengeana uwezo wa kiutendaji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...