Tanzania ina malengo madhubuti katika ushiriki wake kwenye Maonesho ya Kibiashara ya Kidunia Expo 2025 Osaka Japan kwa kutangaza fursa za biashara, kuvutia uwekezaji na kuonesha urithi wake katika tamaduni na desturi katika maonesho hayo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jaffo wakati akizungumzia umuhimu wa Siku ya Tanzania yaani (Tanzania Day) itakayofanyika tarehe 25 /05/2025 na Kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii litakalofanyika tarehe 26 Mei 2025 zinazolenga kunadi fursa za uwekezaji zilizopo nchini kwa lengo la kuvutia wawezekaji katika sekta mbalimbali ikiwemo maliasili, utalii, kilimo, viwanda na biashara na kutilia mkazo kuhusu fursa kubwa iliyopo katika uwekezaji katika joto ardhi.

Aidha Dkt. Jafo amewakaribisha wadau na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...