RUAHA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM),CPA Amos Makallla amewaomba wananchi wa  jimbo la Mikumi kukiunga mkono chama hicho, katika uchaguzi mkuu .

CPA Makalla ametoa kauli hiyo leo Alhamisi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ruaha Jimbo la Mikumi wilayani Kilosa aliposimama kuwasalimia akielekea Kilombero.

Makalla amesema hapo zamani wananchi wa Morogoro katika majimbo ya Kilombero, Mikumi na Mlimba walionjeshwa sumu, lakini hivi sasa waliowaonjesha( Chadema) hawatashiriki tena.

Kutokana na hilo, CPA Makalla amewataka wananchi wa Morogoro kwa kujiandikisha ili kupata fursa ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ili kukiwezesha cham hicho kupTa ushindi mnono.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoshiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ni  mserereko wa ushindi kwa chama hicho tawala.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...