Na. Josephine Majura, WF, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amesema kuwa miradi 80 imewezeshwa na Serikali na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini, Mhe. Oran Manase Njeza, aliyetaka kujua idadi ya miradi iliyowezeshwa na Serikali kwa utaratibu wa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi.
Alisema kuwa miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali ambapo miradi mitatu ipo katika hatua ya utekelezaji, miradi minne ipo katika hatua ya majadiliano, miradi miwili ipo katika hatua ya ununuzi, miradi 26 ipo katika hatua ya upembuzi yakinifu, miradi 13 ipo katika hatua ya upembuzi yakinifu wa awali na miradi 32 ipo katika hatua ya andiko dhana.
“Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), imeanzisha Mfuko wa Uwezeshaji Ubia (PPP Facilitation Fund – PPPFF), kwa lengo la kuziwezesha Mamlaka za Serikali kuandaa na kutelekeza miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP)”, alisema Mhe. Chande.
Aliongeza kwa Sheria hiyo imekipa Kituo cha Ubia (PPP Centre) jukumu la kutoa usaidizi wa kiufundi kwa Mamlaka za Serikali na Sekta Binafsi wakati wa uibuaji, maandalizi na utekelezaji wa miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Akieleza kuhusu ujenzi wa Barabara ya Igawa – Tunduma kwa utaratibu wa PPP, Mhe. Chande alisema kuwa, kwa sasa yupo mshiriki kutoka Sekta binafsi ambae anaandaa mradi huo kupitia utaratibu wa PPP.
Aidha Serikali ya Tanzania na Zambia zipo kwenye majadiliano na Serikali ya China na mwelekeo ni mzuri na wakati wowote Serikali hizo zitaweka saini makubaliano kupitia Kampuni ya China ya CECC kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Mhe. Chande alisema kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi kwa kuwashirikisha katika hatua za uandaaji wa miradi ili waweze kuwa na mchango katika maendeleo ya nchi na sekta hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Mhe. Oran Manase Njeza, aliyetaka kujua idadi ya miradi iliyowezeshwa na Serikali kwa utaratibu wa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, bungeni, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...