Madaba_Ruvuma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed, amempa mkandarasi anayejenga vyumba vya madarasa 6, matundu ya vyoo 10 pamoja na mabweni 2 katika Shule ya Sekondari Madaba muda wa wiki moja kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huu ambao unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 417 hadi kukamilika, kupitia fedha za mradi wa Barrick.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi, alimuelekeza mkandarasi kuongeza juhudi kwa kuongeza rasilimali watu ili kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati huku akizingatia usafi na ubora unaostahili.
Aidha, ametoa agizo kwa mkandarasi kuanza kutoa taarifa ya maendeleo ya kazi kila siku jioni ili kurahisisha usimamizi na kuhakikisha hatua kwa hatua za utekelezaji zinafuatiliwa kwa ukaribu.
Pia alionya kuwa iwapo mkandarasi huyo atashindwa kutekeleza maagizo hayo, mkataba wake utavunjwa na kazi hiyo kupewa mkandarasi mwingine atakayekuwa tayari kutekeleza mradi kwa ufanisi na kwa viwango vinavyotakiwa.
Mradi huo ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha miundombinu ya elimu Halmashauri ya Madaba, ikiwa ni hatua ya kuinua kiwango cha elimu na mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...