KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025 Ismail Ali Ussi amesema,Serikali imejipanga na itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi ikiwemo ya maji ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye shughuli zao za maendeleo.
Amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mpara Kata ya Likunja Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi baada ya kuzindua mradi wa maji uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(Ruwasa)kwa gharama ya Sh.287,709,840.51.
Amesema,kutekelezwa kwa mradi huo kunatokana na mapenzi makubwa ya Rais Samia kwa Wananchi wa kijiji cha Mpara na Wilaya ya Ruangwa kwa ujumla, na amewataka kuendelea kushirikiana na Serikali kufanya kazi za kujiletea maendeleo ili kupunguza umaskini kwenye maeneo yao.
Amewataka kuhakikisha wanatunza mradi huo na miundombinu yake ili uweze kudumu kwa muda na kutoa huduma endelevu ya majisafi na salama kwenye maeneo yao waliyoikosa kwa muda mrefu.
Aidha,amewapongeza wataalam wa Ruwasa Mkoa wa Lindi kwa kutekeleza vizuri na kwa ubora mradi huo ambao umewezesha Wananchi wa vijiji vitano kupata huduma ya maji ya uhakika na muda wa kujikita kwenye shughuli za kiuchumi.
Katika hatua nyingine Ussi,amewakumbusha wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kuhusu kujiandaa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba Mwaka huu kwa kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la kudumu la Mpiga kura ambazo zitawapa fursa ya kuchagua Viongozi wanaowapenda.
“Ndugu zangu wana Ruangwa,Uchaguzi huu ni muhimu sana kwenu kwani ndiyo utawezesha wapata Viongozi bora watakaowatumikia katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo ambao mtashirikiana nao kuleta maendeleo katika maeneo yenu”alisema Ussi.
Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Ruangwa Lawrence Mapunda alisema,Ruwasa wanatekeleza mradi wa uchimbaji visima vitano na ujenzi wa miundombinu katika vijiji ambavyo havikuwa na huduma ya maji ya uhakika.
Alisema,programu hiyo maalum ya Serikali ya uchimbaji visima 900-5 kwa kila Jimbo inayotekelezwa nchi nzima ni mwendelezo wa dhamira ya kweli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo kichwani na Wilaya ya Ruangwa inatekelezwa katika vijiji vya Mmawa,Mtawilile,Njawale,Mpara na Namkatila.
Alisema,kabla ya mradi huo Wananchi wa Vijiji hivyo walikuwa wanapata huduma ya maji kupitia visima vifupi na visima vya asili ambavyo vilifanya kazi kipindi cha masika na vilikuwa mbali na makazi yao kwa wastani wa kilometa 1 hadi 5.
Alieleza kuwa,vyanzo vya maji vya mradi huo ni visima vyenye uwezo wa kuzalisha maji kati ya lita 4,900 na lita 13,200 kwa saa na kisima kilichochimbwa katika Kijiji cha cha Mpara kina uwezo wa kuzalisha maji lita 4,900.
Alisema,lengo la kujenga mradi wa maji Mpara ni kumaliza changamoto ya maji iliyokuwepo kwa muda mrefu na kupitia mradi huo sasa wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama karibu na maeneo yao.
“Jumla ya kaya 970 zenye wakazi 4,850 wa Vijiji vitano wanapata majisafi na salama na mradi huu unaendeshwa na kusimamiwa na Wananchi wenyewe kupitia vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya Jamii(CBWSO) na Wananchi wanachangia Sh.50 kwa ndoo moja ya lita 20”alisema Mapunda.
Mkazi wa Kijiji cha Mpara Amina Juma,ameishukuru Serikali kuwajengea mradi wa maji ambao umemaliza changamoto ya majisafi na salama na kero ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 1 kwenda kutafuta maji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...