Mdhamini mkuu wa Ligi ya NBC Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa timu ya Azam FC (U20) ya jijini Dar es Salaam baada ya timu hiyo kuibuka bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025 kufuatia ushindi wake wa goli 1 – 0 dhidi ya wenzao Foutain Gate (U20).

Shujaa wa Azam FC (U20) jana alikuwa ni mshambuliaji Carlos Chasambi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 11 ya mchezo.

Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Bw Joseph Lyuba aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kwenye tukio hilo lililopambwa na uwepo wa mashabiki na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Lyuba alivipongeza vilabu shiriki vya ligi hiyo hususani mshindi timu ya Azam FC (U 20), mshindi wa pili Fountain Gate FC (U20), mabenchi ya ufundi pamoja na TFF huku akielezea namna ambavyo ushindani kwenye ligi hiyo umeboreka, hatua ambayo kwa mujibu wake inathibitisha muelekeo mzuri katika ukuaji wa mchezo wa soka hapa nchini.

“Msukumo wa NBC kudhamini ligi hii ya vijana unachagizwa na dhamira yetu ya kuwa na ligi kuu yenye ubora na ushindani kutokana na vipaji vinavyozalishwa hapa nchini. Tunaamini ili tuwe na Ligi Kuu ya NBC yenye mvuto na ushindani lazima tuanzie katika ngazi hii ya kuibua vipaji. Tunashuru kuona hili linaenda vizuri na matunda yake yataonekana zaidi kwenye ligi za NBC Championship, ligi Kuu ya NBC na hata timu ya Taifa,’’ alisema Lyuba.

Kwa mujibu wa Lyuba, Benki hiyo imejipanga zaidi kuendelea kuboresha udhamini wake kwenye ligi zote tatu inazozidhamini ili kuongeza kasi ya ushindani, kuboresha hadhi ya ligi hiyo, kuchochea ajira pamoja na kuboresha hali ya maisha ya wadau mbalimbali waliopo kwenye mnyororo wa mchezo huo ikiwemo wachezaji na mabenchi ya ufundi.

Akizungumzia mashindano hayo, Kocha Mkuu wa Azam FC (U20), Kassim Liogope pamoja na kuwapongeza wachezaji wake, uongozi wa timu hiyo, TFF na mdhamini benki ya NBC, alisema mashindano hayo yaliambatana na ushindani mkubwa hususani katika hatua ya nane bora kutokana na timu shiriki kubadilika kiuchezaji hatua ambayo inathibitisha uborekaji mkubwa wa viwango vya ubora wa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara Benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Bw Joseph Lyuba (alievaa fulana nyeupe) akikabidhi kombe la Ligi ya NBC ya Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) kwa nahodha wa timu ya Azam FC (U20) Ismaily Ally baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2024/2025. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam kufuatia mechi ya fainali baina ya mabingwa hao na wenzao kutoka Fountain Gate FC (U20). Mechi hiyo iliisha kwa timu ya Azam FC (U20) kuibuka na ushindi wa 1-0. Anaeshuhudia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (alievaa kofia)


Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara Benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Bw Joseph Lyuba (wa pili kulia) sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (alievaa kofia), Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya (kulia) wakiongoza zoezi la uvalishaji wa medali kwa wachezaji wa timu ya Azam FC (U20) baada ya timu hiyo kuwa bingwa wa Ligi ya NBC ya Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) msimu wa 2024/25 Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam kufuatia mechi ya fainali baina ya mabingwa hao na wenzao kutoka Fountain Gate FC (U20). Mechi hiyo iliisha kwa timu ya Azam FC (U20) kuibuka na ushindi wa 1-0.






Wachezaji wa timu ya Azam FC (U20), viongozi na wadau mbalimbali wakijipongeza baada ya timu hiyo kukabidhiwa rasmi kombe la ubingwa wa Ligi ya NBC ya Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) msimu wa 2024/2025. Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo ilifanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam kufuatia mechi ya fainali baina ya mabingwa hao na wenzao kutoka Fountain Gate FC (U20) mechi hiyo iliisha kwa timu ya Azam FC (U20) kuibuka na ushindi wa 1-0.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (kulia) pamoja Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara Benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Bw Joseph Lyuba wakifuatilia mechi ya fainali ya kombe la Ligi ya NBC ya Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) kati ya timu ya Azam FC (U20) na Fountain Gate FC (U20). Mechi hiyo iliisha kwa timu ya Azam FC (U20) kuibuka na ushindi wa 1-0.


Vikosi vya Azam FC (U20) na Fountain Gate FC (U20) vilivyochuana kwenye fainali hiyo.


Mtanange ukiendelea! Shujaa wa Azam FC (U20) jana alikuwa ni mshambuliaji Carlos Chasambi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 11 ya mchezo.


Muonekane wa Kombe la Ligi ya NBC ya Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) 2024/25



Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC, Mdhamini mkuu wa Ligi ya NBC Vijana chini ya miaka 20 (NBC U20 Youth League) wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Biashara Benki ya NBC ambae ndio Mwenyekiti wa kamati ya Ligi Kuu ya NBC ndani ya benki hiyo, Bw Joseph Lyuba (Katikati) wakijipongeza wakati wa hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa huo iliyofanyika jana katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...