Na Philomena Mbirika, Dodoma

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imewezesha ushiriki wa vikundi vya ufugaji vyuki katika maadhimisho ya siku ya Nyuki Duniani yanayofanyika viwanja vya Chinangali Park Dodoma kuanzia tarehe 17 hadi 20 Mei 2025 yakiwa na kauli mbiu isemayo Nyuki kwa uhai na uchumi Imara, tuwahifadhi”

Akizungumza katika Banda la NCAA kwenye maadhimisho hayo Askari wa Uhifadhi Mkuu Flora Patta kutoka sehemu ya Maendeleo ya Jamii, alisema kwamba shughuli za ufugaji nyuki zinazoratibiwa na NCAA zinahusisha kuwezesha vikundi vya wafugaji nyuki kwa kutoa Mizinga, Mafunzo na kuwaungalisha na Masoko ya ndani na nje kupitia majukwaa mbalimbali.

“ Shughuli hizi za kuwezesha wafugaji nyuki ni sehemu ya mikakati ya hifadhi katika kuleta dhana ya uhifadhi shirikishi kupitia shughuli ambazo ni rafiki kwa mazingira ambapo hadi sasa NCAA imetoa jumla ya mizinga ya Nyuki 3,179 kwa vikundi 125 vilivyopo Jirani na ndani ya Hifadhi kwa Wilaya za Karatu, Meatu, Monduli na Tarafa ya Ngorongoro” alisema Flora

Aidha Flora alisisitiza kuwa kupitia shughuli za ufugaji nyuki, NCAA imewezesha wawakilishi wa vikundi vya Nyuki viwili kutoka vijiji Vya Rhotia kati na Khainam kushiriki maadhimisho hayo ambapo wamekuja na bidhaa mbalimbali zinazotokana na ufugaji Nyuki zikiwemo Asali,Dawa ya Kikohozi, Sabuni, Nta, Kiwi ya Viatu na nyingine nyingi.

Bw. Stephen Marco kutoka Kijiji cha Rhotia kati, ambaye ni mmoja wa wanakikundi aliyeshiriki kwenye maadhimisho hayo, alisema kwamba wamefurahi kupata fursa kuuza bidhaa zao na kujifunza kutoka kwa wadau wengine wa ufugaji nyuki ambapo hii ni hatua muhimu kwao katika kuboresha ufugaji wao na kuongeza kipato cha familia zao.

“Sisi tumekuwa tukijihusisha na shughuli za ufugaji nyuki na kwa sasa tumeweza kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na ufugaji wa Nyuki ambazo tumekuja nazo kwa ajili ya kuuza na sisi tupate fursa ya kujifunza zaidi kutoka kwa wenzetu” Alisema Stephen

Maadhimisho haya ya Siku ya Nyuki Duniani yamekusanya wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo watafiti, wakulima, taasisi za serikali na mashirika binafsi, wote kwa pamoja wakijadili namna bora ya kukuza sekta ya ufugaji nyuki sambamba na kuhifadhi mazingira.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...