Farida Mangube, Morogoro
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini amevitaka vyama vyote vya siasa kuhakikisha vinafuata sheria na kanuni za maadili ya uchaguzi wakati wa kampeni, siku ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi, ili kulinda amani na utulivu wa taifa.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Morogoro na Msaidizi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA).
Nyahoza alisema kuwa ni wajibu wa kila chama cha siasa kuhakikisha kinaeneza ujumbe wa siasa za kistaarabu na kushiriki katika uchaguzi kwa kufuata misingi ya kisheria na kidemokrasia.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NRA, Hassan Kisabya Almas, alisema chama hicho kimepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake, ikiwa ni pamoja na kushiriki chaguzi zote kuu na ndogo, pamoja na kuongeza idadi ya wanachama kutoka 189,237 hadi kufikia 307,934 kwa sasa.
Almas aliongeza kuwa NRA imeweza kufungua matawi 203 na ofisi sita za mikoa ambazo zinatoa huduma katika mikoa ya Dar es Salaam, Tabora, Dodoma, Pemba na Unguja.
"Tunazingatia maadili ya Kitanzania kabla, wakati na baada ya uchaguzi. NRA si chama cha matusi wala kejeli. Sisi ni chama cha siasa, kazi yetu ni siasa. Upinzani huanza baada ya uchaguzi," alisema Almas.
Katika mkutano huo, mwanachama Mariam Hamadi Hassan kutoka Zanzibar alikabidhi zawadi kwa chama chake kama ishara ya kuthamini kazi kubwa inayofanywa na NRA katika kuwaunganisha wanachama wa Bara na Zanzibar ambapo alipewa ofa ya kutumika kutangaza sera za chama na mgombea urais katika kipindi chote cha kampeni kwa kuwa ameonesha utayari wa kukitumikia chama.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa chama kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.ukiwa na ajenda kuu ya kumteuwa mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Munggano wa Tanzania na mgombea Uras wa Zanzibari.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...