Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeshiriki Kongamano la Tatu la Umoja wa Vijana wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT), lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kongamano hilo limebeba kaulimbiu “Vijana, Fursa Kidigital na Artificial Intelligence (AI)” na limewakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kuwapa uelewa kuhusu teknolojia mpya na nafasi ya akili bandia katika maendeleo ya taifa.

Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa TACAIDS, Dkt. Catherine Joachim, ambaye alisisitiza umuhimu wa vijana kutumia teknolojia kwa ubunifu na ustawi wa jamii.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkaguzi wa Ndege Nyuki kutoka TCAA, Bw. Ibrahim Abdallah, alieleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya nchi ya udhibiti wa ndege nyuki, mtu yeyote haruhusiwi kutumia ndege hizo iwapo hazijasajiliwa na Mamlaka. Aidha, ndege nyuki zinazoingizwa nchini zinatakiwa kuwa na kibali maalum cha kuingia kabla ya kufika mipakani.

Bw. Abdallah alibainisha pia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na matumizi ya ndege nyuki, zikiwemo shughuli za kilimo, uchimbaji madini, mapambano dhidi ya ujangili na wanyama waharibifu, udhibiti wa uvuvi haramu, pamoja na usambazaji wa dawa katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi kutokana na changamoto za miundombinu ya barabara.

TCAA kupitia ushiriki wake, imesisitiza dhamira ya kushirikiana na vijana katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya kisekta kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Mkaguzi wa Ndege Nyuki kutoka TCAA, Bw. Ibrahim Abdallah akiwasilisha mada ya ufahamu wa ndege zisizo na rubani wadau mbalimbali wa IT wakati wa kongamano la Tatu la Umoja wa Vijana wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT), lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa TACAIDS, Dkt. Catherine Joachim  akifungua kongamano la Tatu la Umoja wa Vijana wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT), lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali pamoja na wanachuo wa vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT) wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Tatu la Umoja wa Vijana wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...