Serikali itaendelea la kutoa mafunzo ya Mtaala uliboreshwa kwa walimu wote nchini ili kuhakikisha wanakuwa bora katika eneo la ufundishaji na ujifunzaji shuleni.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa elimu nchini , Dkt. Lyabwene Mutahabwa aliyemwakilisha mgeni rasmi , Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tkenolojia, Prof. Carolyne Nombo kwenye uzinduzi wa mafunzo ya walimu wa ajira mpya wa somo la Elimu ya Biashara ulioboreshwa leo tarehe 27/5/2025 katika chuo cha Ualimu, Mkoani Tabora.

Dkt. Mutahabwa amesema, uzinduzi huu ni tukio muhimu kwa walimu nchini ambapo mafunzo hayo yatawasaidia katika kupata mbinu za kufundisha somo hilo ambalo litawezesha wanafunzi katika kufanya biashara na kuwataka walimu hao kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini.

“Nawasishi sana mzingatie mafunzo haya mtakayopewa na wawezeshaji kwani baada ya kuboreshwa kwa Mtaala, somo la Elimu ya biashara ni jipya hivyto hapa mtapata mbinu za kufundisha na pia hakikisheni mnakuwa na upendo na kujitambua katika kazi yenu.” Amesema Dkt.Lyabwene.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba amesema, kwa kutambua umuhimu wa mafunzo katika kufanikisha utekelezaji wenye ufanisi wa mitaala, Serikali ya awamu ya sita imeipatia TET jumla ya shilingi 9,940,000,000 ili kukuza Sekta ya Elimu nchini kupitia eneo la mafunzo.

"Kwa kutambua umuhimu wa mafunzo katika kufanikisha utekelezaji wenye ufanisi wa mitaala, Taasisi ya Elimu Tanzania imepokea jumla ya shilingi 9,940,000,000." Amesema Dkt. Komba

Aidha, Dkt. Komba ameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia TET fedha kutekeleza majukumu yake yakiwemo utoaji wa mafunzo na uandaaji na usambazaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserekali la EDUCATE, Bw. Nelson Musikula amesema, kama wadau wataendelea kutoa ushrikiano katika kuinua elimu nchini hasa katika somo la elimu ya biashara ili kuwezesha wanafunzi wote nchini wanapata uelewa na kuweza kujifunza namna ya kuanzisha biashara.

Mafunzo hayo yamejumuisha washriki kutoka mikoa saba ambayo ni Kigoma, Katavi, Mwanza, Geita, Rukwa, Kagera na wenyeji Tabora huku lengo ni kiwafikia mikoa yote nchini.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...