.jpeg)
WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi, ajira, vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameshiriki Kongamano la watu wenye ulemavu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar lililoandaliwa na Ikupa Trust Fund kama mgeni rasmi akimuakilisha Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko naibu waziri mkuu na waziri wa nishati, kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar, Dodoma Mei 09,2025,
Kupitia kongamano hilo Mhe. Ridhiwani amewahakikishia Washiriki utayari wa serikali kushirikiana nao katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kushiriki shughuli zote za kijamaa ikiwemo kujenga uchumi na kujenga Jamii itakayopambana kwa ajili ya maslahi mapana ya Wenye Ulemavu,
Katika hatua nyingine Mhe. Kikwete amepokea mchango wa Tsh milioni moja kutoka kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya uchukuzi wa fomu ya kugombea urais ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi mkuu unaotajiwa kufanyika mwaka huu,
Mhe. Kikwete amekabidhi vifaa wezeshi kwa makundi hayo ya watu wenye ulemavu, mafuta chupa 103 ya tshs 2,060,000/= , Miwani ya jua 38 ya tshs 190,000/=, Magongo 91 ya thamani 4,550,000/=, Fimbo nyeupe kwa wasioona 36 za tshs 1,260,000/=, Kofia 27 za tshs 405,000/=, ambavyo vyote vina zaidi ya thamani ya shilingi milioni nane,
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mhe. Kikwete amewakumbusha Watu wenye Ulemavu kuwa nao ni sehemu ya nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo sawa na wasio na ulemavu na hii ndiyo imekuwa dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...