Serikali imedhamiria kuendelea na mwelekeo wa kimkakati wa kuwekeza katika maeneo yenye uwezo wa kukuza uchumi jumuishi na shindani, hasa kupitia sekta ya usafiri.
Lengo kuu ni kurahisisha biashara, kuvutia uwekezaji wa ndani na nje, na kuwaunganisha wazalishaji na masoko kwa maendeleo endelevu ya taifa.
Akizungumza leo MEI 19, 2025 katika Maonesho ya kibiashara jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Benki ya Equity Tanzania, Mkuu wa Chuo Cha Biashara (cbe), Profesa Tandi Luoga, akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Suleiman Jaffo, alisisitiza umuhimu wa kutumia urithi wa asili na tamaduni za Tanzania katika kukuza utalii na kuvutia wawekezaji katika sekta za malazi, usafiri, na huduma za kijamii.
'Ni muhimu kutumia vyema urithi wa asili na tamaduni zetu, Tanzania kwani inaweza kujipambanua duniani kama kivutio kikuu cha utalii na pia kama eneo lenye fursa nyingi za uwekezaji katika malazi, usafiri, na huduma za kijamii,na kuwa kujiunganisha na masoko ya kikanda kupitia EAC na AfCFTA kunatoa nafasi ya kukuza biashara na kuvutia mitaji mipya". Alisema Profesa Luoga
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Isabela Maganga alieleza kuwa mkutano huo ni jukwaa muhimu la kuunganisha wadau na kufanikisha uwekezaji unaoendana na vipaumbele vya taifa na ajenda ya AfCFTA.
Alibainisha kuwa zaidi ya wajumbe 236 kutoka Afrika, Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati walishiriki, ishara ya kuongezeka kwa mvuto wa mazingira ya biashara Tanzania. Alisisitiza dhamira ya benki hiyo kusaidia uwekezaji, hasa kwa biashara zinazoendeshwa na wanawake na vijana.
Kwa upande wake, Oscar Kisanga, Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, alisema chemba hiyo kwa kushirikiana na serikali imeanza kuwaelimisha wafanyabiashara wa ndani kuhusu umuhimu wa kuchangamkia fursa ya soko la pamoja la Afrika (AfCFTA) ili kujikwamua kiuchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...