Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jafo amesema kuwa kwa mwaka 2025/26 Kiwanda cha mbolea Minjingu kilichopo Mkoani Manyara kina mpango wa kuongeza mitambo ya uzalishaji mbolea ya kukuzia ya NPK hadi kufikia tani 400,000 kwa mwaka kutoka tani 59,600 za mbolea aina ya phosphate.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari akielezea mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia.

Ambapo amesema kwa sasa mahitaji ya mbolea ni tani milioni 1 ambapo zaidi ya asilimia 60 ni mbolea ya chumvi chumvi ambayo huagizwa kutoka nje ya nchi, na kusema kuwa uzalishaji unaendelea kuimarika ambao unatajiwa kuwa ni zaidi ya tani milioni 1 kwa mwaka ili kupunguza uagizaji wa mbolea hasa ya chumvi chumvi kutoka nje.

"Kiwanda cha mbolea cha minjingu kilichupo Mkoani Manyara kimewekeza Shilingi Bilioni 50 na kina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha tani 250,000 za mbolea kwa mwaka".

"Hadi kufikia machi 2025 kiwanda kimezalisha tani 59,600 za mbolea aina ya Phosphate ambazo ni sawa na asilimia 23.84 za uwezo uliosimikwa. Kiwanda kimetoa ajira 200 za moja kwa moja na ajira 560 zisizo za moja kwa moja,Aidha kwa mwaka 2025/2026 kiwanda kina mpango wa kuongeza mitambo ya kuzalisha mbolea ya kukuzia ya NPK hadi kufikia tani 400,000 kwa mwaka"

Aidha Dkt Jafo ameleeza kuwa hadi kufikia machi 2025 uzalishaji wa sukari ya matumizi ya kawaida ulikuwa tani 446,332 katika viwanda vyake 7 ikiwemo Mtibwa Sugar Limited na Kilombero Sugar Company Limited ambapo mahitaji ya sukari nchini ni tani 900,000 kati hizo tani 650,000 ni kwa matumizi ya kawaida na tani 250,000 ni kwa matumizi ya Viwandani sambamba na kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

"Tanzania ina viwanda saba vya sukari ikiwemo Kilombero Sugar Company Limited na Mtibwa Sugar Limited,viwanda hivi vya sukari vimetoa ajira za moja kwa moja takribani 34,200 na ajira zisizo za moja kwa moja 200,000 aidha viwanda hivyo vina uwezo uliosimikwa kwa kuzalisha sukari tani 638.486.6 kwa mwaka ambapo mahitaji ya sukari nchini ni tani 900,000 kati ya tani hizo,tani 650,000 ni kwa matumizi ya kawaida na tani 250,000 ni kwa matumizi ya viwandani. Hadi kufikia machi 2025 uzalishaji wa sukari ya matumizi ya kawaida ulikuwa tani 446,332".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...