Brussels, 21 Mei,2025
Tanzania na Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuendeleza ushirikiano wa kimkakati baina yao.
Makubaliano hayo yamefikiwa katika Kongamano la Bajeti la Umoja wa Ulaya lililofanyika jijini Brussels Ubeligiji ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo.
Akizungumza katika Kongamano hilo lililokuwa likijadili vipaumbele vya bajeti ya EU kwa kipindi kijacho.
Mhe. Nyongo ameshukuru kwa ubia mzuri uliopo baina ya Tanzania na EU na akaeleza kuwa Tanzania imejipanga kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inalenga kufikia Pato la Taifa (GDP) la dola za Marekani trilioni moja.
Mhe. Nyongo ametoa rai kwa Umoja wa Ulaya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji katika maeneo ya kipaumbele kama vile nishati, miundombinu, kilimo na madini.
"Tunauona Umoja wa Ulaya kama mshirika wa kweli wa maendeleo. Ushirikiano wetu siyo tu kama mfadhili wa muda mfupi, bali ni wa kimkakati kwa manufaa ya pande zote mbili" Amesema Mhe. Nyongo.
Tanzania imealikwa katika kongamano hili kama nchi pekee kutoka Afrika kushiriki kutokana na mahusiano mazuri ya muda mrefu na Umoja wa Ulaya.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...