NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
BENKI ya Biashara ya Tanzania (TCB) imejipanga kuendeleza mageuzi ya kidijitali ili kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, lakini katika upande wa ukuaji wa mizania ya kifedha, jumla ya mali za benki ziliongezeka kwa asilimia 25 hadi kufikia shilingi trilioni 1.74, na amana za wateja zilifikia shilingi trilioni 1.17, ikiwa ni ishara ya kuongezeka kwa imani ya wateja.
Haya yameelezwa leo Mei 26, 2025 jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCB Martin Kilimba katika Mkutano Mkuu wa 33 wa wanahisa uliofanyika katika ofisi za TCB.
Amesema benki hiyo inaweka mkazo kwenye kuboresha miundombinu ya teknolojia ya kidijitali na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa makundi hayo muhimu ya uchumi, kwa lengo la kuchochea maendeleo ya sekta binafsi na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
Amesema katika mwaka huu wa fedha, wanakusudia kuendelea kuboresha ufanisi ili kuwezesha ukuaji wa taasisi hii.
"Malengo yetu ni kuendelea kuboresha mizania, kujenga taswira mpya ya taasisi yetu, kutumia fursa zinazoletwa na teknolojia ya kidijitali, kufanya uhakiki wa hasara, pamoja na kusimamia rasilimali watu". Amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Adam Mihayo amesema benki hiyo imetengeneza faida ya Shilingi bilioni 44 kabla ya kodi katika mwaka wa fedha uliopita huku akisisitiza kuwa kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea.
"Benki imetengeneza faida ya Shilingi bilioni 44 kabla ya kodi pia mapato yasiyo na riba yameongezeka, benki pia imeweza kuokoa asilimia 10 ya fedha iliyopangwa kutumika". Amesema Mihayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...