NA Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

MTENDAJI.Mkuuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wahasibu wa Mahakama hapa nchini kuzingatia mafunzo ili kwenda kuondoa dosari ndogo ndogo zinazobainika kwenye ripoti ya CAG kwa upande wa mahakama.

Pia amewataka wahasibu hao,ambao hawana CPA kwenda kuongeza elimu ili kuzidi kupanua wigo wa taaluma hiyo kutokana na mambo kubadilika.

Prof.Gabriel amesema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya Wahasibu wote wa mahakama nchini yaliyofanyika jijini Dodoma chini ya wataalamu kutoka PWLC

Amesema mafunzo hayo ni ya muhimu sana kwa wahasibu hao,kwa sababu wanahitaji kuzidi kupata hati safi kwenye ripoti ya CAG ambayo hutolewa kila mwaka kwa taasisi mbalimbali hapa nchini ili wawe mfano bora.

Prof. Gabriel amesema kutokana na hilo aliwataka washiriki kusikiliza kwa makini kile ambacho wanakwenda kufundishwa ili waende kukifanyia kazi kwa vitendo katika maeneo wanayotoka.

"Naomba muwe watulivu kwenye wakati wa mafunzo nahitaji kuona kila mmoja anatoka na kitu mara baada ya mafunzo hayo ya siku mbili,"alisema Profesa Ole Gabriel.

Hata hivyo aliwapongeza wahasibu wote kutoka mahakama zote hapa nchini waliohudhuria mafunzo hayo huku akiwasisitiza wasimilize kwa makini ikiwemo kuuliza maswali pale ambapo hawajaelewa.

"Kama mnavyofahamu hivi sasa mambo yanabadilika kila iitwapo leo na nyie mjenge utaratibu wa kujisomea ili muende sambamba na mageuzi kwenye kutumia teknolojia,"alisema Prof Ole Gabriel.

Amesema mahakama ya Tanzania imefanya maboresho makubwa kwenye miundombinu hivyo na wao kwenye taaluma ya Uhasibu wanapaswa kuwa mfano ikiwemo kuishauri mahakama kuhusu mifumo ya kitumia.

Mbali na hilo aliwataka wahasibu hao,kujiendeleza ili.wawezankuchukua masomo ya CPA Kwa sababu kwenye taaluma ya uhasinu CPA ina umuhimu mkubwa sana hivyo ambao hawana hiyo wakasome.

Naye Mkurugenzi wa Fedha wa Mahakama ya Tanzania Joseph Elikana alissma aliswma kwenye taaluma ya uhasibu kuna mambo yanabadilika kila iitwapo leo hivyo usipojenga utaratibu wankujisomeana itakupa tabu katika baadhi ya vitu kwenye uhasibu.

Amesema wahasibu wanapaswa.kujifunza mambo mapya kila mara kwa sababu taaluma hiyo inabadilika kila mara kwenye baadhinya mambo kama viwango.

"Bila mafunzo ya kawaida, wahasibu wanaweza kushindwa kutoa ushauri mzuri kwa sababu ya ukosefu wa maarifa juu ya mambo mbalimbali yanayobadilika kwenye taaluma hiyo,"alisema Elikana.

Hata hivyo alimshkuru Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa kuwezesha mpango wa mafunzo hayo ambayo yana faida kwa wahasibu hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...