Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imesaini mkataba wa mashirikiano wa miaka mitatu na Shirika lilsilo kiserikali la EdTech katika eneo la akili mnembe (AI) utaosaidia ujifunzaji na ufundishaji ili kuboresha Sekta ya Elimu nchini.
Mkataba huo umesainiwa baina ya Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba na Mkurugenzi wa EdTech Bw. Essa Mohamedali leo Mei 9, 2025 katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akieleza baada ya kumalizika kwa tukio hilo Dkt. Komba amesema, TET imepanga kufanya mafunzo ya kukuza uwezo kwa wakuza mitaala na walimu nchini kwa kutumia Akili Mnemba (AI) ili kukuza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.
"Haya ni mapinduzi makubwa kwa hatua zinazoendelea kupigwa, kwa sasa duniani kuna maendeleo makubwa sana katika sayansi na teknolojia, kwahiyo matumizi ya AI katika ufundishaji na ujifunzaji yatampunguzia sana mzigo mwalimu," amesema Dkt. Komba.
Aidha, Dkt. Komba amesema lengo ni kuhakikisha idadi kubwa ya walimu nchini wanaoweza kutumia teknolojia hiyo wanafikiwa katika kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji, na kwamba katika Mtaala mpya wataingiza kipengele cha kutumia AI.
Naye, Mkurugenzi wa Tanzania AI Community, Essa Mohamedali, amesema wamefurahi kushirikiana na Taasisi ya Elimu kwakuwa wataweza kuwaongezea uwezo walimu wote nchini na kuwafanya watekeleze vizuri zaidi majukumu yao.
"Tuko hapa kwaajili ya kuwapatia walimu zana muhimu zitakazowasaidia kufundisha wanafunzi kwa ufanisi zaidi, na tunafurahisana kushirikiana na TET katika kuhakikisha AI inatumika kuleta mapinduzi ya elimu nchini," amesema Mohamedal.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...