*NCC kuhakikisha vinadhibiti utoro, hasara kwa matengenezo ya kila wakati

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), lililo chini ya Wizara ya Ujenzi, imetekeleza ahadi yake kwa kuhakikisha viwango na viwango msawazo vya ujenzi bora wa majengo ya shule zake za awali, amali na sekondari vinaandaliwa, ili sekta husika ya elimu ivizingatie au kuvitumia pindi inapoandaa miongozo ya ujenzi wa shule, pamoja na ununuzi wa samani kwa ajili ya shule hizo.

NCC imefanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa ujenzi, wahusika wa uboreshaji na matengenezo ya mifumo ya umeme, maji na huduma nyingine muhimu kutoka katika wizara na taasisi mbalimbali, kwa kuandaa rasimu, baada ya kupitia miongozo inayotumika sasa, kuichambua na kuangalia changamoto au mapungufu yaliyopo, hususan kwenye eneo la viwango na viwango msawazo vya ujenzi wa shule na aina ya samani zinazotumika.

Kwa mujibu wa Mratibu wa maandalizi ya viwango na viwango msawazo hivyo, Mhandisi Heri Hatibu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa NCC, lengo la kuandaa viwango na viwango msawazo hivyo ni kuweka muongozo wa usanifu, ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya shule za Serikali.

“Tunafanya hivyo ili kuhakikisha kunakuwa na viwango na viwango msawazo vya ujenzi wa majengo ya shule vinavyoendana na wakati uliopo wa sayansi na teknolojia, vyenye kuzingatia mahitaji halisi ya watumiaji wa majengo, wakiwemo wenye mahitaji maalum, na vyenye kuzingatia usalama wa wanafunzi, walimu na mazingira” Mha. Hatibu amesema.

Aidha, ameongeza kuwa, viwango hivyo vinavyotarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2025/2026, vitasaidia kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimali za nchi, yatakayowezesha kupangwa bajeti za usimamizi wa miradi ya ujenzi, kwa urahisi.

Wakati akifungua kikao kazi cha kuandaa viwango hivyo mjini Morogoro hivi karibuni, Mtendaji Mkuu wa NCC, Mha. Dkt Matiko Mturi amesema, inapaswa viandaliwe viwango na viwango msawazo vitakavyo rejesha ujenzi wa majengo mbalimbali yakiwemo ya shule, kwenye ubora unaotakiwa, unaozingatia usalama na kuendana na thamani halisi ya gharama zinazotumika, kama ilivyokuwa zamani.

Dkt Matiko anasema, ukiangalia majengo yaliyojengwa miaka mingi iliyopita utagundua kuwa ni bora na hayahitaji matengenezo ya mara kwa mara kama yanayojengwa sasa. Amesema ujenzi wa majengo hayo ulizingatia mambo mengi muhimu ambayo miongozo yetu mingi ya sasa haiyaainishi.

“Ukiangalia maabara za shule zilizojengwa zamani utagundua kuwa za sasa zina walakini. Lakini, si maabara tu, bali hata majengo ya shule za zamani za Serikali ni imara. Kwa sababu hiyo, ninasisitiza muandae viwango na viwango msawazo vitakavyosaidia kuandaliwa kwa miongozo ya ujenzi wa shule hizo, itakayo ondoa mapungufu hayo,” amesema. 

Mha. Ronald Mwajeka wa Idara ya Maendeleo ya Miundombinu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ametaja baadhi ya mapungufu yaliyopo katika viwango na viwango msawazo vilivyopo kwenye miongozo inayotumika katika ujenzi wa shule za serikali, ambayo yamepatiwa ufumbuzi kuwa ni Maeneo yaliyokuwa na changamoto na kupatiwa suluhisho kwa kuwekewa viwango ni pamoja na uchaguzi wa eneo/maeneo ya ujenzi, vigezo stahiki vya kuzingatia katika kutekeleza ujenzi, vielelezo vya kuzingatia wakati wa usimamizi na ukaguzi wa kazi za ujenzi.

 Mengine ni eneo la ubora na uimara wa vifaa vinavyotumika katika ujenzi, kuwekwa kwa viwango vya chini vitakavyozingatiwa wakati wa ujenzi, kuhakikisha kuwa jengo linaweza kutumika na watu wa hali zote. Amesema awali viwango havikugusia shule za amali lakini vya sasa vimezizingatia.

kmtaalamu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Agricia Mtakyawa amesema viwango na viwango msawazo vinavyo andaliwa  vitapunguza matumizi ya fedha za Serikali kwenye huduma za maji, umeme na nyingine, kwa sababu vimeelekeza ujenzi utakaoruhusu uvunaji na uhifadhi wa maji ya mvua, pamoja na matumizi zaidi ya nishati ya umeme wa jua.

“Majengo ya shule yatazingatia ukubwa wa madirisha unaoruhusu hewa na mwanga wa kutosha, taa za umeme zinazotumia ‘sensor’ ambapo panapokuwa na mtu darasani zinawaka zenyewe na kujizima pindi wanafunzi na walimu wote wanapotoka darasani, au bwenini, ofisini kwa wanaohusika na maeneo hayo.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...