Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha imewataka Wafanyabiashara mkoani hapo kuhakikisha kwamba wanajenga utamaduni wa kufanya makadirio ya kodi na kulipa kodi zao stahiki kwa wakati.
Hayo yamesemwa leo 24 Mei, 2025 na Afisa Msimamizi Kodi Mkuu wa TRA, Bw. Flavian Byabato wakati wa mwendelezo wa Kampeni ya utoaji elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango yenye lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara mkoani hapo kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, ikiwemo kusikiliza kero zao za kikodi na kuzitatua.
Bw. Byabato amesema kuwa, Baadhi ya Wafanyabiashara mkoani hapo wamekua wakijisahau kufika katika ofisi za TRA kwa ajili ya kufanyiwa makadirio ya kodi jambo ambalo halileti tija katika masuala ya ukusanyaji wa kodi, hivyo amewahimiza kujenga utamaduni wa kufika kufanyiwa makadirio ya kodi kila muda muafaka wa kufanya hivyo unapofika.
“Tumebaini kuwa, wengi wenu hamfiki kufanyiwa makadirio ya kodi licha ya kukumbushwa mara kwa mara ili muweze kujua kodi stahiki mnazopaswa kuzilipa, niwaombe mjenge tabia ya kufika kwa wakati kwa ajili ya makadirio ya kodi ili kuepuka usumbufu”, alisem Byabato.
Sambamba na wito huo, amewataka wafanyabiashara mkoani hapo kujenga utamaduni wa kutoa risiti halali za EFD kwa kila mauzo wanayofanya au huduma wanazotoa kwani kwa kufanya hivyo kunawawezesha kutunza kumbukumbu sahihi za biashara zao.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara kutoka mitaa ya Kwa Morombo jijini hapo wameeleza kufurahishwa na zoezi la kutembelewa na Maafisa wa TRA na kuwapa elimu ya kodi na kusikilizaa changamoto zao za kikodi ambapo wameiomba TRA kuendelea na utaratibu huo mara kwa mara.
Kampeni ya elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango ni zoezi endelevu linalofanywa na TRA katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaelimisha walipakodi kuhusu masuala ya kodi ili waweze kulipa kodi zao kwa hiari ambapo kwa Mkoa Arusha zoezi hilo bado linaendelea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...