Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha kulea yatima cha  CHAKUWAMA jijini Dar es Salaam.

Msaada uliotolewa na wanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo ni pamoja na unga, mchele, sukari, mafuta ya kula, sabuni na vifaa mbalimbali vya mahitaji ya shule.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo, Mkuu wa shule hiyo iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguri, Edrick Philemon alisema kuna umuhimu kwa jamii kuwakumbuka watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuwapa misaada ya aina mbalimbali.

Alisema imekuwa kawaida kwa kila mwaka shule za St Anne Marie Academy kutoa misaada mbalimbali kwenye vituo vya yatima kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii ambayo ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya shule hizo.

Alisema watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanahitaji upendo wa jamii hivyo hatua ya kuwapa msaada wa vifaa vya shule na vyakula vinawapa moyo kuwa jamii iko pamoja nao.

“Umekuwa utaratibu wetu wa kila mwaka kutoa msaada kama huu kwenye vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na tunaomba jamii iige mfano wa St Anne Marie Academy,” alisema

“Shule yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kuanzia shule ya awali, msingi na sekondari, tunafaulisha na kuwa wa kwanza kitaifa, kiwilaya na hata kwenye kata kwa hiyo mafanikio yote haya lazima turudishe shukrani kwa jamii kwa kutoa misaada kama hii,” alisema

Alisema shule hiyo itaendelea kutoa elimu bora kwa kuhakikisha wanafunzi wake wanaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa kuanzia ngazi ya Kata.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ilivyoweka mazingira mazuri kwenye sekta ya elimu na kuwa karibu na wawekezaji binafsi katika elimu hali ambayo imechangia sekta ya elimu kuendelea kukua,” alisema

Mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho, Edina John alishukuru wanafunzi wa St Anne Marie Academy kwa msaada huo na kuomba jamii kuiga mfano huo.

Alisema watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanamahitaji mengi hivyo hatua ya wanafunzi wa shule hiyo kuamua kuwapelekea msaada imewafariji na kuona kwamba jamii inawajali.






Mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...