*Azindua mradi wa kuimarisha ustahimilivu wa Bianuai ya misitu ya mazingira asili a dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
WAZIRI wa Maliasili na Utalii DK.Pindi Chana amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua katika kuimarisha uhifadhi wa misitu nchini na moja ya hatua muhimu zinazochukuliwa ni kubainisha hifadhi za misitu zenye upekee hususani katika uwepo wa baionuai au zenye kutoa huduma za kiikologia muhimu kama vile maji kwa jamii kubwa na kuzipa hadhi ya juu ya uhifadhi.
DK.Pindi Chana ameyasema hayo leo Mei 5,2025 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bianuai ya misitu ya mazingira asili dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuzindua Mkakati wa Taifa Urejeshaji wa mandhari ya misitu nchini.
Akieleza zaidi katika uzinduzi huo DK.Pindi Chana amesema kuhusu mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuai ya Misitu ya Mazingira Asilia Tanzania dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi unalenga kuimarisha uwezo wa misitu yetu kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema mradi huo utatekelezwa kwa miaka sita kuanzia Septemba 2023 hadi Septemba 2029 kwa gharama ya Dola za kimarekani 5,837,010 ambazo zimetolewa na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kwa pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Pia Mradi unatarajiwa kutekelezwa katika Misitu ya Hifadhi tisa iliyo katika mikoa mitano ambayo ni mkoa wa Pwani, Manyara, Lindi, Ruvuma na Arusha. Mradi huo utaboresha miundombinu ya kuwezesha kufanyika kwa utalii ikolojia kama vile ujenzi na ukarabati wa Barabara.
Ameongeza mradi utahusika ujenzi wa vituo vya ulinzi wa misitu, mabanda ya kupumzika watalii, kuwezesha jamii kuwa shughuli za kuongeza kipato na kujenga uwezo wa wataalam kushiriki katika majadiliano ya biashara ya kabon.
"Tunawashukuru UNDP na watalaam wake wote wa ndani na nje kwa kuwa bega kwa bega katika kazi hii kubwa iliyowezesha nchi yetu kuwa na misitu yenye hadhi hiyo 25 hadi sasa.Kupandisha hadhi misitu hiyo kumekuwa na matokeo chanya kama vile kuimarika kwa uhifadhi misitu hiyo na baionuai ya mimea na Wanyama
"Na kuongezeka kwa shughuli za utalii ikolojia ambapo wageni walikuwa chini ya 10,000 mwaka 2015 ambapo sasa kufikia zaidi ya 250,000 kwa mwaka na mapato zaidi ya Sh.Bilioni 2.Matokeo chanya katika sekta yetu ya utalii yamechagizwa pia na msukumo mkubwa unaofanywa na viongozi wetu akiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia maono na maelekezo yake pamoja filamu ya Tanzania the Royal Tour na filamu ya Amazing Tanzania. "
Amesema pamoja na mafanikio katika uhifadhi hususani misitu hiyo ya mazingira asilia bado matishio ya uharibifu wake unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi makubwa.Ili kupamba na changamoto hizo mradi kama huo ni muhimu nyakati hizi.
Aidha amesema utekelezaji wake unabeba moja kwa moja malengo ya mkakati wa kungoa ardhi ya misitu iliyoharibika.Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na serikali kufanya tathmini ya misitu yetu kubainisha maeneo yenye uhitaji wa kuimarisha uhifadhi kwa kiwango cha juu.
Pia TFS na Wadau wa maendeleo kuendelea kutafuta fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati kama huu kwenye hifadhi nyingine zilizosalia hata kwa awamu, TFS, Idara ya Misitu na Nyuki na Serikali za mitaa kuendelea kuboresha sheria na usimamizi wa misitu katika katika maeneo yao.
DK.Pindi Chana pia amesema ni vema kuhakikisha mradi huo unaleta matokeo yanayokusudiwa ili kujenga Imani ya wafadhili wa mradi huu na miradi ijayo.
Kuhusu Mkakati wa Taifa wa Urejeshaji wa Mandhari ya Misitu Tanzania( 2023 – 2033) amesema nchi yetu ni miongoni mwa nchi 34 za Afrika ambazo hadi sasa zimeshaweka lengo la kurejesha mandhari ya misitu. Mataifa hayo yameweka malengo tofauti ambayo inaongozwa na mikakati mbalimbali.
Amefafanua Tanzania ilijiunga na Mpango wa Afrika wa Urejeshaji wa Mandhari ya Misitu (AFR100) mwaka 2018, na wakajitolea kurejesha hekta milioni 5.2 za ardhi na misitu iliyoharibika kufikia mwaka 2030.Ameipongeza TFS kwa uongozi wake imara katika kusimamia kazi za kurejesha mndhari ya misitu yetu.
Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema wakiwa katika hatua ya uzinduzi wa mradi huo TFS chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)wamekamilisha maandalizi yote muhimu.
Ameongeza na wameanza kwa kasi utekelezaji wa mradi huo huu kwa ufadhili wa Mfuko wa Mazingira ya Dunia awamu ya saba (GEF 7) na unachangiwa kwa kiwango kikubwa na rafiki zao UNDP na taasisi mbalimbali za Serikali.
Profesa Silayo amesema maandalizi ya mradi huo yameanza miaka mitano iliyopita toka mwaka 2018/19-2023/24, hivyo ni wakati muafaka sasa wa kuona mradi waliouandaa u kwa kushirikiana sasa unaanza kutekelezwa.
"Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka sita (6) katika misitu ya hifadhi za mazingira tisa (9) ukiwa na gharama ya Dola za Kimarekani 5,837,010 kitatumika kutekeleza shughuli za mradi huku akifafanua lengo kuu la mradi ni kujenga uwezo wa misitu ya hifadhi za mazingira asilia kuwa stahimilivu na athari za mabadiliko ya tabianchi.
"Inatarajiwa mradi utawezesha miundombinu ya ulinzi wa misitu, vituo vya utalii hasa malango la kuingilia hi madhini na maeneo ya kupumzika.Kuimarisha shughuli za kuongeza mapato kupitia utalii ikolojia na shughuli za kuongeza mapato kwa jamii zinazozunguka misitu.
"Mradi utaimarisha ushirikiano na jamii na wawekezaji wanaozunguka maeneo ya hifadhi katika kubuni na kutekeleza shughuli za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mradi utatekelezwa katika Misitu ya Hifadhi tisa iliyo katika mikoa mitano
Ametaja hifafhi hizo ni Hassama Hills, Nou na Mlima Hanang katika Mkoa wa Manyara, Uzigua na Pugu-Kazimzumbwi Mkoa wa Pwani, Pindiro na Rondo Mkoa wa Lindi, Hifadhi ya Msitu wa Mwambesi Mkoa wa Ruvuma na Hifadhi ya Msitu wa Essimingor Mkoani Arusha."

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...