
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 23, 2025 amewasili Osaka nchini Japan kumwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya kimataifa ya Osaka (World Expo 2025 Osaka).
Akiwa nchini Japan, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.
Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...